ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 20, 2014

DENGUE YAZUA KIZAAZAA UBUNGO, ABIRIA WAKWAMA MASAA MAWILI


Abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea mikoa mbalimbali na nchi jirani kupitia kituo kikuu cha mabasi Ubungo, jijini Dar Es Salaam leo asubuhi wamejikuta katika
wakati mgumu baada ya mabasi kuzuiwa kwa muda wa masaa mawili kutoka kituoni hapo kufuatia madai kwamba baadhi ya wamiliki wa mabasi hayo ya kusafirisha abiria kukaidi agizo la serikali la kupulizia dawa ya kuua mbu wanaoeneza ugonjwa hatari wa dengue.


Hata hivyo mabasi hayo yaliruhusiwa kuendelea na safari baada ya kutekeleza agizo hilo majira ya saa 2 asubuhi.

No comments: