Sifa kwa wanasiasa kokote
duniani ni nadra, hasa kwenye mitandao ya kijamii, lakini watu
wamemmiminia sifa Rais wa Uruguay baadhi wakitamani kama marais wao
wangekuwa kama Rais Jose Mujica wa Uruguay.
Kwenye Twitter kuna zaidi ya ujumbe laki moja wa
watu nchini Uhispania wakitamani kama waziri mkuu wao angekuwa kama
Rais Maskini zaidi duniani Jose Mujica wa Uruguay.
Rais huyo anasifika kwa kuendesha
gari kuu kuu , kuishi maisha ya watu wa kawaida na sehemu kubwa ya
mshahara wake yeye hupatia mashirika ya misaaada ya kibinadamu...kiasi
kwamba anajulikana kama Rais masikini zaidi duniani.
Na ndio maana waziri mkuu wa
Hispania Mariano Rajoy huenda asifurahie sana kufananishwa na Rais wa Uruguay.
Lakini swali ni watu wangapi duniani wanaweza
kufananisha Rais Uruguay na marais wao? Ni Marais wangapi duniani
wanatoa mishahara yao kwa mashirika ya misaada ya kibinadamu, kuishi
maisha ya kawaida na kuendesha gari lililochoka?
Baadhi ya wananchi wanahoji kwa nini nchi kama
Uruguay ambayo haina uchumi mkubwa ina huduma bora zaidi kwa jamii
kuliko Hispania ambayo imekomaa kiuchumi wakati rais wake hana uchu wa
madaraka na tamaa ya pesa?
Mitandao ya kijamii hutumiwa sana kwa mijadala
kama hii. Swali ni je nani ana jambo zuri la kusema kumhusu Rais wake
hasa katika hizi nchi zetu za Afrika? Unadhani kiongozi yupi barani
Afrika anaweza kufananishwa na huyu Rais wa Uruguay? Je kuna Rais
asiyeishi maisha ya kifahari enzi hizi?
BBC
2 comments:
Absolutely!
Mzee wetu, Baba wa Taifa Mwl. Nyerere!
Julius k. Nyerere hakuna ubishi.. ..
Post a Comment