ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 25, 2014

ELIZABETH GURUMO NDIYE MAMA MJASILIAMALI BORA 2014, AZAWADIWA MILIONI TANO

Mgeni rasmi, Ahmed Shikeli, akimkabidhi cheki ya shilingi milioni tano mshindi Elizabet Gurumo.
Elizabeth akiwa ameinyanyua juu cheki yake ya milioni tano mara baada ya kukabidhiwa.
Akina mama waliofanikiwa kuingia tano bora.
Majaji wakiwa kazini.
MC wa shindano hilo, Hadija Shaibu ‘Dida’, akiwa kazini.
Wanamuziki wa Mashauzi Classicc wakiimba kuipambiza hafla hiyo.

5. Mwimbaji wa Mashauzi, Saida Ramadhani, akinengua na wanenguaji wa bendi hiyo.

6. Mwandaaji wa shindano hilo, Moreen Mnyele (kulia) akiwa na mkuu wa majaji.
7. Mgeni rasmi Ahmed Shikeli (kushoto) akiwa na Moreen wakiwa wameshika mfano wa cheki ya milioni tano kwa ajili ya mshindi.
10. Mashabiki wakinengua kwa staili maalum baada ya kutangazwa mshindi.
11. Mshindi akiwashukuru mashabiki.

HATIMAYE Elizabeth Gurumo jana aliibuka kuwa Mama Mjasiriamali Bora kwa mwaka 2014 katika sherehe ya kukata na shoka iliyofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam ambapo karibu kinamama 30 walishiriki.
Katika shindano hilo ambalo bendi ya Mashauzi ilitoa buridani, kinamama watano tu ndio waliingia fainali na mmoja kuibuka kidedea na kujinyakulia zawadi ya shilingi milioni tano.
(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY)

No comments: