ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 22, 2014

Fahamu Sifa za Mwanamke wa Kuoa (Wife Material)

Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachoweza kuwafanya wakapata wachumba ni uzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.
Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtamkia kwamba anataka kumuoa.
  • 1. MWEYE MAPENZI YA KWELI
  • 2.MWENYE TABIA NZURI
  • 3. MWENYE UCHU NA MAENDELEO
  • 4. ASIYEPENDA MAKUU
  • 5. MVUMILIVU
Mwanamke ukiwa na sifa hizo tano hapo juu unauwakika wa 100% kuolewa.
Nawasilisha!

6 comments:

Anonymous said...

U have a loong way to go BRODA!!! Jidanganye,wenye ndoa wangapi wana mapenzi ya kweli,kutwa nzima michepuo mpaka wanatia kinyaa.

Anonymous said...

Kwa kweli nakubaliana na hizo sifa hapo huu na kuwa uzuri sura SI tabia. Wazee zamani waliliona hili na ndoa zao zilidumu...siku hizi wanawake wengi wanaangalia maslahi zaidi kuliko mapenzi ya kweli na pindi Yale maslahi yakikosekana au kupungua vinaanza visa na kufanya mke na mume kuanza kutoka nje ya ndoa kwa kushindana..na mwisho wake ndoa huvunjika na endapo wana watoto basi watoto ndiyo watakaoathirika zaidi. Hivyo kabla ya kuoa ni vizuri kumchunguza mwanamke kwa Makini Sana kwani mkiishia kuachana na mkiwa na watoto basi watoto ndiyo watakaoathirika zaidi...

Anonymous said...

Na kumbuka watu wananbadilika. Atakuwa na sifa za kuoa/kuolewa leo akishapata anachotaka mambo yanakuwa mambo. Usijidanganye mwanadamu

Anonymous said...

Dj ndio unatuma maombi ya kutafuta mchepukooo?

Anonymous said...

Bora mwanamke muuza baa, kuliko mvaa ushungi.....siri ya mtungi aijuaye.....????

Anonymous said...

shida adabu yako na adabu ukushike usitukashifu wewe mdau wa at 11:40 am wa mtoa comment mwisho hapa, nakuambia tena shika adabu yako na adabu ikushike kama wewe ndo mlevi au mvuta bangi au kihiyoo basi mwanamke wa baa anakufaa wewe na dini yako huko na kwa aliye siye mlevi wala mvuta bangi basi wa ushungi ndo anayemfaaa na usitutokaniye wanawake zetu wanaovaa ushungi.

hapo hapo ulipofika usione tunakunyamazia tunakujua uliyetoa comment so shika adabu yako vizuri ukingina katika mtandao huu na hangover zako hapa ujuwe utashika adabu zako vizuri