ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 12, 2014

Israel yasaidia Nigeria kuwatafuta wasichana


Jeshi la Nigeria linafanya kila juhudi kuwatafuta wasichana hao ingawa limelaumiwa kwa kujikokota
Kikosi cha Israel cha kukabiliana na ugaidi kinatarajiwa kujiunga na juhudi za kuwatafuta zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara nchini Nigeria na wanamgambo wa kundi la Boko Haram.
Kundi hilo litajiunga na wataalamu wa Marekani,Uingereza na ufaransa ambao tayari wako nchini Nigeria.
Rais Goodluck Jonathan amesema kuwa kujiunga kwa
Israel katika operesheni hiyo ni wazi kwamba dunia nzima inaunga mkono usakaji wa wasichana hao.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kuwa uwepo wa wataalam wa Israel katika oparesheni hiyo huenda kukazua hisia za kisiasa nchini Nigeria ambapo wasiwasi kati ya wakristo wanaoshi kusini mwa taifa hilo na waislamu wanaoishi kazkazini huzua ghasia.
Awali Gavana wa jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo, eneo ambalo wasichana hao walitekwanyara alisema kuwa ana habari kuhusu kule walipo wasichana hao
BBC

1 comment:

Anonymous said...

wenye akili chambueni sana mnavyosoma si unaona janja yao ya kuingia kiulaini nigeria na kuchota mafuta