TANGAZO MAALUM:
Kamati
ya Uchaguzi wa viongozi wa jumuia ya Watanzania DMV imeanza kuandaa utaratibu
na mchakato wa kuwachagua viongozi wetu.
Watanzania sote tunahamasishwa tushiriki kwa umoja katika zoezi hili
adhimu ili tupate viongozi bora
watakaotusogeza mbele kijamii na
kibinafsi.
Kamati
hii inawatambua Watanzania na marafiki
zao wote kwa mujibu wa katiba. Wanajumuia hao kwa pamoja ni:
1)
Wale raia waliolipia ada kamili;
2)
Wale wasio raia wenye mnasaba na wale waliolipia ada kamili; na
3)
Wale raia ambao
hawakulipia ada lakini kwa njia moja au nyingine anajuhusisha na jumuia.
Ni
dhamira ya Kamati kwa mujibu wa katiba
kuwatambua hao wanajumuia kwa kadiri ya ushiriki wao, na hivyo mchakato wa
kupiga kura utatambua michango ya
kila mpiga kura.
No comments:
Post a Comment