TANGAZO
MAALUM:
Kamati
ya Uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV imeundwa
na imeanza kuandaa utaratibu na mchakato wa kuwachagua viongozi wetu. Watanzania wote tunahamasishwa tushiriki kwa
umoja katika zoezi hili adhimu ili tupate viongozi bora watakao tusogeza mbele
kijamii na kibinafsi.
Kamati
hii inawatambua Watanzania na marafiki
zao wote kwa mujibu wa katiba. Wanajumuiya hao kwa pamoja ni:
1)
Wale raia waliolipia
ada kamili;
2)
Wale wasio raia
wenye mnasaba na wale waliolipia ada
kamili; na
3)
Wale raia ambao
hawakulipia ada lakini kwa njia moja au nyingine wanajihusisha na Jumuiya.
Ni
dhamira ya Kamati kwa mujibu wa katiba kuwatambua hao wanajumuiya kwa kadiri ya
ushiriki wao, na hivyo mchakato wa kupiga kura
utatambua michango ya kila mpiga
kura.
Ratiba
kamili ya utaratibu na maagizo mengine kuhusu ugombeaji wa cheo utafuata punde.
3 comments:
".............. 3)Wale raia ambao hawakulipia ada lakini kwa njia moja au nyingine wanajihusisha na Jumuiya.
Ni dhamira ya Kamati kwa mujibu wa katiba kuwatambua hao wanajumuiya kwa kadiri ya ushiriki wao, na hivyo mchakato wa kupiga kura utatambua michango ya kila mpiga kura."
Swali: Hivi Katiba ya Jumuiya ndiyo imetoa "Blank Check" kama hii kwa Kamati ya Uchaguzi?
Asanteni wana DMV. Tunaoba mtujulishe tulipeje au kwa nani hizi ada jamani wengine inatupa shida kuzilipa account ipi hiyo??
Asante
Wasiliana na viongozi wa DMV, ina maana wewe hujui mawasiliano ya viongozi wako?
Go to this website ina maelezo yote ya kufanya malipo na namba za simu za viongozi wako.
http://watanzaniadmv.org/membership.html
Post a Comment