ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 25, 2014

Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band mwanamuziki mpiganaji

Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band mwanamuziki mpiganajialeyepachikwa majina mengi ya utani kutokana na matukio
Unapoutaja muziki wa dansi wa Tannzania maarufu kama "Bongo Dansi" jina la
Mwamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja na mzimu wake
"Ngoma Africa band" aka FFU-Ughaibuni ukipenda waite "Watoto wa Mbwa"
au Viumbe wa ajabu "Anunnaki Elien" yenye makao yake kule Ujerumani.

Mwanamuziki Kamanda Ras Makunja wa FFU-Ughaibuni,tunamtaja kuwa
Mpiganaji na mmoja wa watunzi wachache sana wa muziki dansi ambaye nyimbo au tungo zake zina uzito na ujumbe mkubwa kwa jamii,na maana nyingine
nyimbo zake zinamafunzo fulani,pamoja na sifa hizo mwanamuziki huyu
Kamnada Ras Makunja na mzimu wake "Ngoma Africa Band" ukimsikiliza sana
utagundua kuwa ujumbe ulio katika nyimbo zake mara nyingine haumezeki rohoni,
kwa jinsi unavyolenga au kuzungumzia kero fulani katika jamii ,kwa tabia hizi
yeye na bendi yake wamejikuta wakiitwa "Watoto wa Mbwa" yaani wasione kitu lazima watabwaka !
Mara nyingine Mtunzi huyu Kamanda Ras Makunja aliyeipindia akili kazi yake,anapoona nyimbo zake zimekuwa cheche za moto uwa anapooza

kwa kupeleka ujumbe mzuri kwa jamii wenye kuziteka nyoyo za wengi

na kuweza kuzipiga masaji roho za walio wengi "Bongo Tambarare"

hapo kamanda Ras Makunja na kikosi chake Ngoma Africa Band wanaonekana kuwa watoto wazuri lakini tabia zao ni kama ngozi hazibadiriki wawapo jukwaani ni sawa na askari wa kutuliza ghasia FFU, kwa sababu wanajua

wazi tabia za washabiki wao za kupenda mdundo live wenye kasi kubwa

kwa mtindo huu wamefanikiwa kuteka mamilioni ya washabiki nje na ndani ya ughaibuni.

Ras Makunja na Muzimu wake "Ngoma Africa Band" wapo ndani ya medani
ya muziki wa dansi takribani miaka 21 na kushika chati katika majukwaa

ya kimataifa.

inasemekana Ngoma Africa band ina himaya yake inayoitwa "Anunnaki Empire"

himaya ya viumbe wa ajabu (wasanii na waliowazunguka) katika makao ya bendi,wakiwemo mafundi mitambo ambao kazi yao ni kuhakikisha kila kitu

kinacho fanywa ni " Extraordinary" mpaka mziki wenyewe ni "Extraordinary Bongo Dansi" himaya yao haina uwoga bali inatishia wapinzani wao.

Mwanamuziki Ras Makunja inasemekana hatumii ulevi wa aina yoyote hile wa

kuvuta sigara au kasumba bali ni mtu wa mazoezi makali ya kimwili na kihisia,

mazoezi ambayo watu wengi wanadai kuwa yanamsaidia kuongoza kikosi chake
anaposafiri na kufanya tour ndefu,pengine katika nchi zenye utamaduni tofauti na wa afrika. Kamanda Ras Makunja kufanya nae kazi inabidi uwe mjeshi sio mchezo,kwa sababu hana mdhaa katika kibarua chake.

hivi karibuni inasemekana amesharekodi kibao kipya kinachoitwa " Myonge Mnyongeni ! Haki yake Mpeni" wimbo ambao utatolewa baadaye.

Muziki wa bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya unasikika pia katika tuvoti at www.ngoma-africa.com pia www.reverbnation.com/ngomaafricaband

No comments: