ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 8, 2014

KWA WASANII NA WADAU WOTE WA MUZIKI HAPA BONGO

TATIZO = FURSA

ukiijua hiyo hesabu vizuri maisha kwako yatakuwa bam bam Wasanii wengi kwa kipindi kirefu tumekuwa tunalalamika kuwa tunabaniwa kwenye MEDIA bila kuelewa kwa kifupi tu ukweli wa mambo. Kwa Uchunguzi nilioufanya kwa kipindi cha miaka mitatu hivi nimegundua haya, Watayarishaji au watangazaji wa vipindi kwa siku wanapokea zaidi ya nyimbo 30 kutoka kwenye studio mbalimbali hapa nchini, kwao inakuwa ni vigumu kucheza nyimbo zote kutokana either muda kuwa mdogo wa
vipindi vyao au kuwa na request nyingi za nyimbo ambazo wamekuwa wanazicheza sana.
Swali likaja kwangu nyimbo au video ambazo hazichezwi na ni nzuri tufanye nazo nini ili na hawa wasanii wapate airtime?

SULUHISHO LA TATIZO
Baada ya kuliona tatizo nikapata idea ya kuzunguka kwanza Manispaa zote ILALA, KINONDONI na TEMEKE kuangalia usajili wa vituo vya bodaboda na bajaj zilizosajiriwa kwenye vituo ambazo pia wameweka radio ambazo zinatumia flash na memory cards, Huku nikapata idea ya kuanzisha KITAA RADIO FM ambayo itahusika na kuwasambazia watu hapa muziki ule ambao ulishindwa kupenya radioni muziki wa aina yeyote wa Kitanzania ambao mzuri kusikika na watu
wakaupenda.

Pili, kwenye upande upande wa video napo nikajiuliza ni mabus mangapi yaendayo mikoani ambayo ndani hutoa burudani ya movies , music video nk nikakuta ni zaidi ya mabus 2000 ,ambapo kwa siku kila bus linasafirisha si chini ya abiria 50 Huku nako nikapata idea ya kuanzisha BODA 2 BODA Television ambayo itakuwa inatoa burudani ya music videos zile tu zilizokosa kupewa
Airtime kwa namna moja au nyingine Kwa kusema hayo machache napenda kusema KITAA RADIO FM na BODA 2 BODA TELEVISION imezinduliwa rasmi now chini ya kampuni ya SHOWBIZ DEFINED MEDIA Co LTD

NB ; Huduma hii tutaitoa lakini kutakuwa na uchangiaji wa huduma kwa
wale watakaokuwa tayari
Aksanteni

No comments: