
Juhudi za serikali dhidi ya kundi hilo hazijaonekana kuzaa matunda
Taarifa kutoka nchini Nigeria,
zinasema kuwa mamia ya watu waliuawa katika shambulizi lililofanywa na
kundi la wapiganaji wa Boko Haram katika mpaka wa nchi hiyo na Cameroon
siku ya Jumanne.
Katika mahojiano na BBC kiongozi mmoja wa eneo hilo, Ahmed Zanna, alisema kuwa washukiwa walivamia mji wa Gamboru Ngala, katika jimbo la Borno, na kuwaua takriban watu 300.
Inaarifiwa wapiganaji hao waliwafyatulia risasi watu kiholela katika soko kuu la eneo hilo.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema ilikuwa vigumu kupata taarifa hizo mapema kwa sababu ya changamoto ya mawasiliano katika jimbo hilo hasa kwa sababu eneo hilo liko mbali sana.
Wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa walipata zaidi ya maiti miamoja kutokana na shambulizi hilo.
3 comments:
kwanini wawijisaidiye wao wenyewe hapa wanashida kama nini ajiri tabu homeless kibao na mambo mengi tu wanadijai wanasaidia kumbe wanalo lao moyoni
wanatafuta nji ya kuingia na kuyachukua mafuta ya Nigeria na ndo wao ndo wamewateka hawa watoto haafu sasa hivi wanaingia kwa kwa mgongo wa kutwatafuta watoto kumbe huku wanataka kuchukua mafuta
wanatafuta nji ya kuingia na kuyachukua mafuta ya Nigeria na ndo wao ndo wamewateka hawa watoto haafu sasa hivi wanaingia kwa kwa mgongo wa kutwatafuta watoto kumbe huku wanataka kuchukua mafuta
Post a Comment