Wednesday, May 21, 2014

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MIKUTANO YA MH.WAZIRI WA FEDHA AMBAYE ANAHUDHURIA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AFDB) UNAOFANYIKA KIGALI -RWANDA

Waziri wa Fedha Mh.Saada Mkuya Salum akiwa katika majadiliano na viongozi wa Benki ya HSBC kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere ‘Terminal III’. Majadiliano hayo yalifanyika katika Hotel ya Mills Colonie Mjini Kigali Rwanda
Mh.Saada Mkuya Salum,Waziri wa Fedha akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya HSBC baada ya majadiliano yaliyofanyika katika Hotel ya Mills Colonie Kigali Rwanda.
Waziri wa Fedha Mh.Saada M.Salum akimsikiliza kwa makini Bi.Erika Rubin mratibu wa mfuko wa Mkoba Fund wakati wa mkutano wao uliofanyika katika Hotel ya Serena Mjini Kigali Rwanda. Kulia kwa Mh.Waziri ni Nd.Jovin Rugemarila Afisa anayeshughulikia masuala ya ADB na mbele yake ni Kamishina msaidizi wa Fedha za nje –Wizara ya Fedha Nd.Jarome Bureta.
Mh.Saada Salum Mkuya akiwa kwenye mazungumzo ya faragha na mratibu wa Mkoba Fund Bi.Erika Rubin mara baada ya mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Muhabura Mjini Kigali Rwanda.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedhda Dkt.Silvacius Likwilile akieleza kwa muhtasari yale yaliyojadiliwa katika mikutano ya Benki ya maendeleo ya Afrika inayoendelea Nchini Rwanda. Anayemhoji Katibu Mkuu ni mtangazaji wa TBC Nd. Stanley Ganzel.

No comments: