Mkutano wa Maandalizi kwaajili ya Mkutano utakaofanyika mwakani kuhusu tathmini ya Mkataza wa Kuzuia Usambaaji Holela wa Silaha za Nyukilia ( NPT) unaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, pichani ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akitoa mchango wa Tanzania katika Mkutano huo wa wiki mbili. Aliyekaa nyuma ya Balozi Mwinyi, ni Luteni Dkt. Edward Massala kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) ambaye ni sehemu ya ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu.
Na Mwandishi Maalum
Tanzania imeendelea kusisitiza kwamba, nchi ambazo hazina mpango wa kuwa na silaha
za nyukilia basi ziwe na haki ya kutumia
nyukilia kwa matumizi salama, na pia kupewa misaada ya kiufudi na
uwezeshwaji katika eneo hilo
Hayo yameelezwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi
wakati alipokuwa akitoa maoni ya Tanzania katika mkutano wa
Kamati ya Maandalizi kwaajili ya mkutano
utakaofanyia tathmini
utekelezaji wa Mkataba wa kuzuia usambazaji holela wa silaha za nyukilia ( NPT).
Tanzania inashiriki kikamilifu katika Mkutano
huo wa maandalizi ambao ni wa wiki mbili
na unafanyika Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Wanaoshiriki
mkutano huu ni nchi wanachama wa
NPT pamoja na wawakilishi wa mashirika
yasiyo ya kiserikali (NGOs).
Dhumuni la mkutano huu wa
maandalizi, ni kuaanda dondoo na mapendekezo
yatakayojadiliwa katika mkutano
wa tathmini kuhusu NPT. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika mwakani (2015).
Akizungumza kwa niaba ya
Tanzania, Naibu Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi, amesema,
kama Tanzania na kama ilivyo kwa mataifa
mengi ingepeda kuona silaha za nyukilia
zinatoweka katika uso wa dunia. Lakini
inaamini kwamba kila nchi Tanzania ikiwamo
inayo haki ya kuwa na fursa ya
kutumia nyukilia kwa masuala salama.
Mwakilishi huyo wa
Tanzania, amebainisha kwamba, hakuna asiyetambua madhara ya silaha za nyukilia kutokana matukioa kadhaa
mbayo yametokea huko nyuma yakiwamo
ya Hiroshima.
Akatahadharia kwamba kuna dalili za wazi ya kujirudia kwa madhara hayo kwa
kile alichosema Jumuiya ya kimataifa na hasa kwa nchi ambazo zimejilimbikizia
silaha hizo hazitaki konyesha nia ya kweli ya kuachana nazo.
Akasema, inasikitisha kwamba yale mataifa ambayo yana malimbikizo
ya silaha hizo, yameendelea kushikilia misimamo yao na hata kufikia mahali pa
kutetea uhalali wa kuwa na silaha hizo.
Tanzania ikaeleza
kwamba, silaha za nyukilia si tisho
kubwa kwa nchi za Afrika, kwani tishio kubwa na ambalo linachangia katika uvunjifu wa Amani na upotevu wa maisha ya watu ni silaha ndogo ndogo na nyepesi na
siyo silaha za nyukilia.
Balozi Mwinyi amewahoji
washiriki wa mkutano huo, kwamba ni
dunia ya aina gani
tunayotaka kuwarithisha watoto
wetu kwa kuendelea kukumbatia silaha
hizo za maangamizi.
Akabainisha kwamba Tanzania inaamini katika Mkataba huo wa NPT kwa kile alichosema
utekelezaji wake utaifanya dunia kuwa mahali salama. Na kwamba licha ya kuridhia
mkataba huo, Tanzania pia ni
mwanachama wa mikataba mingine ya
kikanda inayohusu uthibiti wa
silaha za nyukilia.
No comments:
Post a Comment