ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 28, 2014

Mbunge Kirufi (CCM, Mbarali) ataka kuvuruga mkutano wa CHADEMA Mbarali

Mkutano wa CHADEMA ulio fanyika leo Mei 28, 2014, wilayani Mbarali ukiwa na agenda  zifuatazo uliingia dosari pale Mbunge wa Mbarali Mh. Kirufi alipo itisha mkutano eneo hilo hilo ambalo CHADEMA ilibidi wafanye mkutano wao. Ikumbukwe kuwa CHADEMA ilitakiwa kufanye mkutano Mei 25, 2014, lakini polis walizui kwa madai kuwa intelejensia sio nzuri na wakasogeza mkutano siku ya leo Mei 28,2014

Agenda za mkutano zilikuwa kama zifuatazo
-Ushuru ulio pitishwa na madiwani wa CCM wa gunia la mpunga
-Katiba na UKAWA
-Taarifa ya CAG juu ya ubadhirifu wa Billion mbili na million mia nne (2 billion na million 400) fedha za halimashauri


Mkutano huu ulio kuwa ukiongozwa na mwenkiti wa CHADEMA wilaya, Ndg. Peter Mwashiti, na kuhudhuriwa na Madiwani wote wa CHADEMA wilayani Mbarali uliingia dosari na kuchelewa kuanza pale ambapo Mbunge wa Mbarali Mh. Kirufi alivyo itisha mkutano eneo moja karibu na mkutano wa CHADEMA.

Uongozi wa CHADEMA wilayani Mbarali ulipo ona Mbunge huyo kaitisha mkutano; ulienda polis na kuonana na OCD kuomba kibali cha uhalali wa Mbunge Kirufi kufanya mkutano siku moja na eneo moja la mkutano wa CHADEMA. OCD aliomba apewe muda na uongozi wa CHADEMA ili aongee na RPC. Baada ya maongezi ya muda mrefu na RPC, OCD alikili kuwa Mbunge kirufi alikuwa afanye mkutano wake siku nne zilizopita, Mei 24, 2014 na hana uhalali wa kufanya mkutano siku ya leo.

Baada ya majadiliano hayo, OCD alitoa amri kuwa Mbunge Kirufi asitishe mkutano wake. Mh. Kirufi alitii amri hii na CHADEMA iliendelea na mkutano wake kama kawaida. Mkutano wa CHADEMA ulimalizika kwa amani na wanaMbarali wakiwa wamepata muongozo juu ya UKAWA, ushuru wa gunia na ubadhirifu wa billion mbili na million 400.


Mwenyekiti wa CHADEMA, Wilayani mbarali Ndg Peter Mwashiti anatoa shukrani za dhati kwa wote walio hudhuria mkutano huo.
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Mbarali, Peter Mwashiti


Habri; Nickodemas

No comments: