Wednesday, May 21, 2014

Mhadhiri MUHAS aigusia DDT katika kutokomeza malaria

Wanasayansi nchini wameshauri serikali kuwekeza zaidi katika kinga kukabiliana na ugonjwa wa malaria nchini na sio kuwekeza fedha nyingi katika dawa.

Wameeleza kuwa nchi nyingi duniani wameweza kukabiliana na ugonjwa huo kwa kupuliza dawa ya DDT. 

Hayo yalielezwa hivi karibuni katika kongamano la wanasayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Mhadhiri wa chuo kikuu hicho, Profesa Kisali Pallangyo alisema mataifa yote yaliyofanikiwa wamewekeza katika kuua vimelea vya mbu na kuzuia malaria na sio katika dawa za kutibu. Alisema licha ya serikali kupambana na ugonjwa huo kwa kugawa vyandarua, wananchi wengi hawavitumii. 

Naye Mhadhiri mwingine wa chuo hicho, Dk Billy Nganda alishauri wafadhili kubadili sera katika kujadili masuala ya Afya kwa kuzungumza na wataalamu ili kuwaeleza maeneo ya kuwekeza kulingana na hali halisi ya nchi. 

Alisema kwa kutumia sera mpya itawezesha wataalamu kushauriana na wizara namna ya kuwekeza kukabiliana na malaria kwa kuua vimelea na siyo kutumia dawa.

No comments: