ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 21, 2014

Vifo vya bomu Nigeria vyafikia 118


vifo vyazidi Nigeria
Maafisa nchini Nigeria wamesema kuwa wamepata maiti 118 kufuatia shambulio la bomu katika mji wa Jos.
Mabomu mawili yalilipuka mojawepo ikiwa imefichwa ndani ya
gari na kulipuka katika soko moja kubwa. Dakika 20 baadaye mlipuko wa pili ulitokea karibu na hospitali.
Inahofiwa kuwa kuna maiti zaidi zilizonaswa kwenye vifusi vya majengo yaliyo poromoka kutokana na shambulio hilo.
mlipuko wa bomu Nigeria
Kufikia sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo lakini wengi wanaamini kuwa Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram lilihusika.
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amejitokeza kukemea mashambulio hayo na kusema kuwa amejitolea kuangamiza kabisa ugaidi.

Mji muhimu

Mji wa Jos unatazamiwa kuwa mji mkuu wa jimbo la Plateau ambalo liko katika eneo la katikati linalo tenganisha kaskazini iliyo na raia wengi zaidi wa kiislamu, na kusini lililojaa wakristu zaidi.

No comments: