ANGALIA LIVE NEWS

Friday, May 23, 2014

MSIBA! MPIGA PICHA MKONGWE WA TV AFARIKI DUNIA!-GPL

Maximilian Ngube 'Max', enzi za uhai wake.

Max (kushoto), akiwa katika moja ya kazi zake enzi za uhai wake. Kulia ni mwanahabari mwenzake.

Mpiga picha mkongwe wa Televisheni, Maximilian Ngube 'Max' amefariki dunia leo, Ijumaa Mei 23, 2014, jijijini Dar es salaam. Habari zilizothibitishwa na ndugu wa karibu wa marehemu zimesema kuwa msiba uko nyumbani kwa marehemu Boko, jijini Dar na mipango ya mazishi inafanyika ambapo tarehe ya maziko itatangazwa baadae.

Marehemu amewahi kufanyia kazi vituo kadhaa vya televisheni nchini, vikiwemo vya Star TV na Mlimani TV ambako ndiko alikuwa hadi kifo kinamkuta. Kazi ya mwisho ya mtandao huu kufanya na marehemu ilikuwa kwenye tuzo za Mwanamke wa Mwaka mjini Dodoma Machi 29, 2014.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEPONI - AMEEN!

No comments: