Lazaro Nyarandu
Mmoja wa waathirika wa Operesheni Tokomeza, anatafuta msaada wa kisheria kuifikisha serikali mahakamani imlipe fidia kwa mateso yaloiyomsababisha kupoteza nguvu za kiume.
Operesheni hiyo iliyolenga kuwadhibiti majangili wa meno ya tembo, ilifanyika mwaka jana nchini, lakini ikakosolewa kwa kusababisha mateso, unyanyasaji na mauaji kwa raia wasiokuwa na hatia.
Muathirika huyo, Peter Ndekeja (45) aliiambia NIPASHE kuwa askari waliotekeleza operesheni hiyo, walimtesa kiasi cha kumpotezea uwezo wa nguvu za kiume, hivyo kumfanya ashindwe kutimiza baadhi ya mahitaji ya ndoa.
Ndekeja ambaye ni diwani wa kata ya Sakasaka (CCM) wilayani Meatu, alidai kuteswa kwenye kambi maalum ya Adajega iliyopo ndani ya hifadhi ya Serengeti, upande wa wilaya ya Bunda mkoani
Mara.
Ndekeja, alisema miongoni mwa adhabu alizopewa ni kulazimishwa kubusu na kufanya mapenzi na mti,
hali iliyomsababishia maumivu kwenye viungo vya uzazi huku baadhi ya sehemu zake za siri zikipasuka.
Mbali na tukio hilo, alidai kuwa pamoja na wenzake kadhaa waliokamatwa, walilazimishwa kufanya mapenzi kwa staili ya nyoka, wakikumbatiana, kupigana busu na kuviringika mithili ya mnyama huyo.
Ndekeja, alisema hivi sasa ndoa yake ‘haina thamani’ kiasi cha kumfanya afikirie kujiua.
Hata hivyo Ndekeja anayedai kuwa afya yake inadorola, amekuwa akipata ushauri nasaha kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki zake.
Anasema, anahitaji taasisi zinatoa msaada wa kisheria na utetezi wa haki za binadamu, wamsaidie ili serikali imtendee haki.
Ndekeja, anaomba pia kukutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira, James Lembeli kwa madai kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu hajaonesha nia ya kumsaidia tangu walipokutana Januari mwaka huu, alipokuwa Naibu Waziri.
Muathirika huyo alikutana na Nyalandu, alipotembelea kata ya Sakasaka, ambapo pamoja na mambo mengine, alitoa hundi ya malipo ya fidia kwa wafugaji walioathiriwa na operesheni hiyo wilayani Meatu.
Ndekeja, mwenye mke na watoto watano alikamatwa Oktoba 7 mwaka jana, kisha kuachiwa huru chini ya amri ya mahakama mwanzoni mwa mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment