Wabunge Kanda ya Ziwa wakamata bajeti yake
Suala la UDA nalo laibuka,lamkera kujadiliwa

Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe
Nguvu ya Kanda ya Ziwa ilimkaba koo Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe juu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, ambao unaelezwa kujengwa kwa kusuasua.
Wa kwanza kumkaba koo Dk. Mwakyembe ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, ambaye aliamua kuondoa shilingi kwenye bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2014/15 kwa kile alichosema kudharauliwa kwa watu wa kanda ya ziwa kwa kuwa wao ni ‘Wasukuma’.
“Mheshimiwa Naibu Spika uwanja huu unaachwa hivi kwa kuwa sisi ni…” alisema bila ya kumalizia sababu hiyo hadi Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo (UDP), alipomalizia kwa kusema kuwa uwanja huo umetekelezwa kwa kuwa wao ni Wasukuma.
Chenge pia aliungwa mkono kuondoa shilingi hadi wapete maelezo ya jinsi fedha zitakazopatika na Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa, alisema hata mshauri mwelekezi anaidai wizara mamilioni ya fedha.
Mbunge wa Busanda, Lourencia Bukwimba (CCM), naye aliunga hoja ya kuondoa shilingi, akitaka maelezo juu ya ujenzi wa uwanja huo.
Mbunge huyo alishauri suala hilo lirudishwe kwenye Kamati ya Bajeti ili fedha zaidi za uwanja huo zipatikane.
Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje (Chadema), pia aliunga mkono hoja hiyo.
Moto huo ulimwibua, Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, ambaye alisema anaunga mkono suala hilo kuangaliwa na Kamati ya Bajeti.
Pia alisema Hazina itatoa Sh. bilioni 6.4 kabla ya mwaka huu wa fedha kwisha ili kupunguza madeni ya wakandarasi wa uwanja huo.
Saada pia alisema watakutana na Kamati ya Bajeti kuangalia uwezekano wa kuongeza fedha kwa ajili ya uwanja huo.
Baada ya maelezo hayo, Chenge alirejesha shilingi hiyo baada ya kuahakikishiwa na serikali kuwa fedha zaidi zitapatikana.
Kadhalika, Mbunge wa Nzega, Dk. Hamisi Kingwangalla aliibua upya hoja ya UDA akitaka maelezo ya serikali hasa baada ya Wizara ya Mwakyembe kuwadai haihusiki na suala hilo.
Alipotaka suala hilo lijadiliwe kwa kuwa kauli ya Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima kudai kuwa suala hilo siyo la wizara hiyo, aliibuka Mbunge wa Mwibara (CCM), Kangi Ligola, aliyewasilisha waraka maalum ambao unaonyesha wizara ya Mwakyembe kuhusika na UDA.
Mjadala wa UDA ulichemka kwa kuwaibua baadhi ya wabunge wakitaka uchunguzi wa uuzaji wa UDA ufanyike ili ijulikane kama iliuzwa kihalali kwa kampuni ya Simon Group.
Awali Kingwangalla akitoa shilingi alisema kama suala hilo litazidi kupotoshwa na kuaharibu sifa ya kamati yake ya Tamisemi atajiuzulu wadhifa wa uenyekiti.
Naye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alishangazwa na tabia ya wizara za serikali kutokuwasiliana na kuwa na kauli tofauti ambazo zinaonyesha kuvuana nguo hadharani.
Mbowe alisema suala hilo serikali ilimalize katika utaratibu wake wa ndani bila ya kuabishana kwani wakazi wa Dar es Salaam wanachotaka ni usafiri bora.
Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Utatibu na Bunge), William Lukuvi, alisema suala hilo limepelekwa Takukuru kwa ajili ya uchunguzi.
Akichangia hoja hiyo, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba, aliishangaa serikali kujitia hawamjui Simon Group kwa sababu hata magari 300 aliyoingiza yalipewa msamaha wa kodi na serikali.
Akijibu hoja za wabunge, Waziri Mwakyembe, alisema anasikitika kwamba suala ambalo linahusisha Wiazara ya Miundombinu wakati huo linaletwa kwenye wizara yake.
Alisema wizara yake haijawahi kupokea suala lolote la UDA mezani kwa ajili ya kutolea uwamuzi na kumuhoji Naibu Spika Ndugui kwanini ameruhusu suala hilo lijadiliwe katiuka wizara yake ambayo haihusiki.
Hata hivyo, Naibu Spika, Job Ndugai, alionyesha kutokubaliana na lawama za Mwakyembe kwamba suala hilo limeruhusiwa kimakosa kwani linahusu uchukuzi ambalo wizara husika haiwezi kilikwepa.
Mwishowe Kingwangalla alirudisha shilingi.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment