Monday, May 19, 2014

MWANAMKE SUDAN KUCHAPWA BAKORA 100 KISHA KUNYONGWA AKISHAJIFUNGUA MTOTO WAKE


Mwanadada Meriam Yahia Ibrahim, ambaye amehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kubadili dini na kuwa Mkristo huko nchini Sudan, imeelezwa kwamba adhabu dhidi ya mwanamke huyo itatekelezwa mara baada ya mwanamke huyo ambaye ni mjamzito wa miezi nane atakapojifungua.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa zinasema kwamba Meriam aliyekana kurudi katika dini yake ya kiislamu hata alipopewa siku tatu za
kutafakari uamuzi wake, imeelezwa kwamba mara baada ya kujifungua atachapwa viboko 100 kisha kunyongwa kwa makosa ya kuikana dini yake ya awali na mbili ni kosa la uzinzi, kwakuwa anamtoto wa kiume mwenye takribani miaka miwili ambaye alimzaa katika ndoa yake ya Kikristo na mumewe daktari Daniel Wani, jambo ambalo kwa dini ya kiislamu hawamtambui mtoto huyo, kwakuwa hakuzaliwa ndani ya misingi ya dini yao.

Kwa mujibu wa Meriam ambaye anaishi gerezani pamoja na mwanae huyo wa kiume toka alipokamatwa mwezi february mwaka huu, amesema hawezi kuachana na imani yake mpya ambayo imekuwa ikimuongoza toka mama yake mzawa wa Ethiopia alipomuongoza kumjua Mungu baada ya kukimbiwa na baba yake mzazi mwislamu kutoka Sudan akiwa na umri wa miaka sita.

Kwa upande wa mime wake daktari Wani imeelezwa kwamba amechanganyikiwa kwasasa asijue la kufanya kutokana na maisha yake yote amekuwa akimtegemea mkewe huyo na kudai kwamba hajui afanye nini kwasasa zaidi ya kumuomba Mungu. Aidha wawakilishi wa balozi za nchi mbalimbali zilizopo nchini Sudan zimeitaka serikali ya nchi hiyo, kumuachia na kumtendea haki Meriam kwa kufuata uhuru wake wa dini katika kuabudu.

Soma kilichotokea kwa kubonyeza HAPA

1 comment:

Anonymous said...

Ndio hii kitu Zanzibar wanataka baada ya kujiondoa kwenye muungano..