Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akipokea kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani, Bw. Herve Ladsous Medali ya Dag Hammarskjold kwa niaba ya mashujaa 10 watanzania waliopoteza maisha mwaka jana huko Darfur na DRC. Nyuma ya Balozi ni Lt Kanali Wilbert Ibunge, Mwambata Jeshi Uwakilishi wa Kudumu.
Sehemu ya wageni waliohudhuria hafla hiyo ambayo awali ilitanguliwa na uwekaji wa Shada la Maua kwa heshima ya mashujaa hao
Hii ndiyo Medali wanayopewa walinzi wa amani ambao wamepoteza maisha wakitekeleza jukumu lao la kulinda amani, Medali hii hupewa Familia ya Marehemu si ya kuvaa bali ni ya kuweka nyumbani
Bango lenye Majina ya Walinzi wa Amani 106 ambao wamepoteza maisha mwaka 2013 wakati wakitekeleza dhamana ya ulinzi wa Amani chini ya Mwamvuli wa Umoja wa Mataifa. Kati ya walinzi hao 106 wamo watanzania 10
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza wakati wa hafla ya siku ya Kimataifa ya kuwakumbuka na kuwaenzi walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa, pamoja na 106 waliopoteza maisha mwaka jana, kumbukumbu hiyo hufanyika Mei 29 kila mwaka. Katika Salamu zake, Katibu Mkuu ameeleza kwamba hupata wakati mgumu sana kumtaarifu Mwakilishi wa Kudumu wa nchi ambayo Mlinzi wake wa Amani au Walinzi wake wa Amani wamepoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao.
Balozi Mwinyi akisaini kitabu na nyuma ni Lt Kanali Wilbert Ibunge
No comments:
Post a Comment