Tuesday, May 20, 2014

Ndege ya Uingereza yaharibikia Nigeria


Ndege ya Uingereza iliyoharibikia kazini na kulazimika kutua Senegal ili kutengezwa
Ndege ya kijasusi ya Uingereza iliyokuwa katika harakati za kutafuta zaidi ya wasichana miambili waliotekwa nyara nchini Nigeria, imelazimika kutua nchini Senegal kutokana na hitilafu.
Ndege hiyo iliondoka Uingereza Jumapili kujiunga na juhudi za kimataifa za kuwatafuta wasichana waliotekwa nyara na Boko Haram na sasa imetua nchini Senegal kutengezwa.
Waziri wa ulinzi wa Uingereza mjini London amesema kuwa ndege hiyo ambayo iliondoka Uingereza Jumapili kusaidia wanajeshi wa Nigeria kuwasaka wasichana waliotekwa nyara, nchini Nigeria zaidi ya mwezi mmoja uliopita.
Wasichana hao walitekwa nyara zaidi ya
wiki tano zilizopita na kundi la wapiganaji waisilamu la Boko Haram.
Nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Marekani na Israel zinasaidia jeshi la Nigeria kwa ujasusi katika harakati za kuwasaka wasichana hao ambao Boko Haram inataka serikali ya Nigeria ibadilishane na wafungwa wa kundi hilo.
Jeshi la Marekani linatumia ndege zenye rubani na zile zisizo na rubani kusaidia juhudi za Nigeria kuwatafuta wasichana hao

1 comment:

Anonymous said...

Kichwa cha habari hakiendani na habari yenyewe. soma vizuri
Iwe vipi ndege iharibikie Nigeria ikatue senegal?