ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 19, 2014

SAHIHISHO:JESSICA MUSHALA NA ISMAIL MWILIMA NDIO WAGOMBEA WA NAFASI YA KATIBU MKUU CCM DMV

Jana Vijimambo iliandika Mama Jessica Mushala ndiye katibu mkuu mpya wa CCM DMV habari hiyo ilikuwa makosa na usahihi ni Mama Jessica Mushala na mwenyekiti wa Vijana Ismail Mwilima ndio watakaokuwa wagombea wa nafasi ya katibu mkuu kweye uchaguzi utakaofanyika June 15, 2014 majina ya Jessica Mushala na Ismail Mwilima yalipitishwa kwenye mkutano wa Halmashauri ya tawi la CCM DMV uliofanyika jana Jumapili May 18, 2014. Katika picha ni mwenyekiti wa tawi ndugu George Sebo (kushoto) na katibu mwenezi na itikadi mama Salma Moshi (kulia) wakiwanyanyua mikono wagombea. Vijimambo inaomba radhi kwa usumbufu wote uliotokea.

5 comments:

Anonymous said...

Hongera mama mushala naona sasa Tawi limepata Jembe ccm yeee.

Anonymous said...

Huyu mama mimi namsupport kwani tunataka kuona effective leadership! Akisema mwakani tunakwenda kigoma kusaidi basi mtakuwa KIGOMA,, KINA MAMA OYEEEEEEEE, mimi si mwana CCM lakini vyama vyote vikipata watu wanaotaka kuleta mageuzi na hali duni ya watanzania nyumbani kitapata wanachama wengi TUMECHOKA VIONGOZI WANAOJIPUBLISH WENYEWE MABLOGINI NA MAPARTY YASIYOKWISHA. WATU WANAKUFA NYUMBANI WATOTO ELIMU DUNI HAKUNA WALIMU WALA VITABU, SO LETS MAKE A DIFFERENCE. Kina mama wa CCM mchagueni huyu mama YOU WILL NOT REGRET

Anonymous said...

Hivi watanzania tuliokuwa huku tumelogwa? Badala ya kukazania kufanya mambo ya maana tunaanzisha vitawi vya CCM/CHADEMA huku kwenye nchi za watu. Mbona wao hawaanzishi vyama vyao huko Tanzania au kwingineko? Kuna mambo mengi sana ya kufanya huku kuliko huo ushabiki wa vyama usio na faida kwa watanzania zaidi ya kujipendekeza tu. Hakuna nchi nyingine zenye wananchi wake wenye vyama nje ya nchi zao zaidi ya watanzania. TUNAPATA FAIDA GANI ZAIDI YA KUENDELEZA USHABIKI USIO NA MAANA?

Anonymous said...

Wewe kalale mpaka nchi zingine ndiyo tuige vipi wewe ?? Wewe siukae kimyaa kama upendi kwasababu wewe upendi basi wote hatupendi??? Get lost mazafantaz

Anonymous said...

Knowledge is power! Elimika uelewe!