ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 26, 2014

TIMU YA VIJIMAMBO INATOA SHUKURANI

Timu ya Vijimambo inapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadau wote walioshiriki na hatimae kufanikisha shamrashamra za memorial weekend zilizofanyika kwa mara ya kwanza DMV.

Shukurani zetu za pekee ziuendee Balozi zetu Washington, DC na New York bila kuwasahau wachezaji wa timu ya New York na DMV kwa kukubali kwao kucheza mechi ya kirafiki na ya kihistoria na ya kwanza kufanyika kati ya haya majimbo.
Timu ya Vijimambo inatoa pole kw mchezaji wa New York, NY Ebra aliyeumia kwenye mechi hiyo mwishoni wa kipindi cha kwanza baada ya kugongana na mchezaji wa DMV tunashukuru Mungu madhala hayakuwa makubwa sana na kwa sasa anaendelea vizuri na ameisharudi New York kwa atayependa kumtembelea na kumpa pole address yake ni 702 E 37th St, Brooklyn, NY 11203 au unaweza kumpigia simu 347 475 4313

Pia tuapenda kuwashukuru wadau wote walioshiriki kikamilifu na kuhahikisha shamra shamra hizi zinafanikiwa shukurani za pekee kwa Abdilahi Makeo na kamati yake nzima bila kumsahau Jacob Kinyemi, Jabir Jongo na Salim Akida. Timu ya Vijimambo tutaendelea kushirikiana siku hadi siku na Tunasema asante na mwenyezi Mungu awazidishie.

No comments: