ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 12, 2014

UKAWA WASAMBAA KWENDA NCHI NZIMA KUANZIA KESHO KUTWA,A MAANDAMANO NA MIKUTANO

Katibu mkuu wa CHADEMA dk WILBROAD SLAA akizungumza na wanahabari mapema leo juu ya ziara yao ya nchi nnzima

Umoja wa katiba ya watanzania UKAWA leo umejitokeza na kutangaza rasmi ratiba yao ya kuzunguka nchi nzima kwa lengo la kutoa elimu juu ya katiba mpya na mchakato huo ulipofikia 
Akizungumza na wanahabari ndani ya makao makuu ya CUF katibu mkuu wa CHADEMA dk WILBROD SLAA amesema kuwa ukawa sasa imeanza rasmi kufanya maandamano na mikutano nchi nzima kila kona ya Tanzania kwa lengo la kuwafikia wananchi na kuwaeleza ukweli kuhusu mchakato wa katiba 
Katibu mkuu wa NCCR mageuzi MOSENA NYAMBABE akizungumza ambaye ni mmoja kati ya viongozi wa ukawa ambao watazunguka nchi nzima

Dk SLAA anasema kuwa kwa wale ambao wanasema kuwa UKAWA ni nguvu ya soda wanapotea kwani muungano huo haujaja kwa bahati mbaya kwani wamejipanga kuhakikisha kuwa inawaleza watanzania ukweli juu ya katiba na jinsi chama cha mapinduzai CCM wanavyoupotosha umma juu ya mchakato huo.

Aidha dk SLAA amesema kuwa kauli ambazo zilitolewa na viongozi wa juu wa chama cha mapinduzi CCM kuwa Tanzania haiitaji sana katiba mpya ni kauli za mtu ambaye hajafika darasani na ni kuwapotosha watanzania na kauli hizo zinatakiwa kupigwa vita sana kwani zinaupotosha umma.
JULIUS MTATIRO akizungumza
Wanahabari mbalimbali wakiwa wanasikiliza kwa makini mkutano huo wa ukawa na wanahabari

UKAWA wametangaza kufanya maandamano na mikutano kona zote za Tanzania kwa kuigawa Tanzania kwa kanda tatu ambazo ni KANDA YA KATI,KANDA YA KASKAZINI,NA NYANDA ZA JUU KUSINI,ambapo viongozi kutoka vyama vitatu wakiwemo makatibu wakuu wote wataongoza mikutano hiyo ambayo itaanza rasmi tarehe 14 mwezi huu.
Credit:Matukio na Vijana

2 comments:

Anonymous said...

Wananchi wanayo mengi muhimu ya kuyafanya kuliko kupotezewa muda wao na nyie wenye tamaa ya uongozi. Mikutano na maandamano yenu haileti chakula mezani kwa wananchi. Kazi yenu kubwa ni kusambaza hofu na kuligawa Taifa. Go to hell UKAWA idiots!

Anonymous said...

Tunashukuru kuwa bado kuna mwenye uchungu na nchi hii. Mdao hapo juu huna uchungu wowote na taifa lako. Unafurahia sana kuona wenzako tukipigwa mabomu,rasilimali zetu zikigawanywa kwa wageni , shule mahospitali yetu yakididimia huku viongozi wakitibiwa India, ujinga na uzembe wa kutupwa katika uongozi wa nchi hii hadi aibu. Wafurahia kulipa rushwa, kunyanyaswa, kudharauliwa, kubakwa, kuteswa, hata kuuawa na vyombo vya dola vinavyotegemezwa kwa kodi yako? Nchi hii haina katiba, utu, wala heshima kwa sasa. Kama una mtoto au mjukuu fikiri mara mbili. Acha kuchumia tumbo tu kizazi kijacho kitalitandika kaburi lako. Mungu tuongezee mwungano. Mungu bariki UKAWA na yote wafanyayo kutetea wanyonge wa nchi hii ambao ndio wengi.