Yadaiwa kutumika kufanya siasa

Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa Wama
Mjadala kuhusu Shirika lisilo la kiserikali liitwalo Wanawake na Maendeleo (Wama), umeliteka Bunge jana ambapo kambi rasmi ya upinzani Bungeni, imeitaka serikali kueleza hatua ilizochukua dhidi ya taasisi hiyo kwa madai ya kutumika kama mwavuli wa serikali kufanya siasa.
Waziri Kivuli wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salum Khalfan Barwany, alisema Wama ambayo Mwenyekiti wake ni Mama Salma Kikwete, mke wa Rais Jakaya Kikwete, imekuwa ikijihusisha na siasa kinyume cha sheria.
Alisema Wama ilituhumiwa ndani ya Bunge mwezi Aprili, mwaka 2012, kuwa ilitumika kisiasa na Mama Kikwete kwenye kampeni za Uchaguzi za mwaka 2010 kwa lengo la kumsaidia aliyekuwa mgombea urais wa CCM wakati huo, Jakaya Kikwete.
Barwany alisema mwaka 2012 Waziri Sophia Simba, wabunge waliomba mwongozo juu ya suala hilo kwa Spika kuwezesha hatua kuchukuliwa lakini hadi leo Bunge halijatoa mwongozo.
"Serikali inayoongozwa na CCM imekuwa ikiyafuta Mashirika yasiyo ya kiserikali yasiyofungamana na chama chochote pale inapoona yanafanya harakati za kudai haki kwa niaba ya makundi mbalimbali ya kijamii kama lilivyofutwa Baraza la Wanawake Tanzania (Bawata) na Shirika la Vijana la National Youth Forum (NYF)," alifafanua.
Mwaka 2012, Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, aliibua hoja hiyo ya kutaka Mama Salma achukuliwe hatua kwa kuwa ni mmoja wa watu ambao wanatumia vibaya asasi zisizo za kiraia (NGO’s) hivyo kutaka awe wa kwanza kuwajibishwa.
“Mheshimiwa Spika naitaka serikali itoe tamko hapa kuwa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama) inayoongozwa na mke wa Rais itakuwa ya kwanza kuchunguzwa na kuwajibishwa kutokana na kuwa ilihusika katika kipindi cha uchaguzi mwaka 2010 kwa kufanya kampeni,” alihoji Mnyika.
Hoja ya Mnyika ilitokana na swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu Ester Bulaya (CCM) aliyetaka kujua serikali inatoa tamko gani baada ya kuwepo kwa tetesi juu ya baadhi ya asasi za kimataifa hapa nchini kuacha majukumu yao na kufanya kazi za kisiasa.
Waziri Simba alimtetea mke wa Rais kuwa hakufanya kampeni kwa kutumia taasisi ya Wana na badala yake alifanya kampeni kama mke wa mgombea.
“Si kweli kwamba Mama Salma alifanya kampeni kwa kutumia asasi yake bali kilichotokea ni kwamba yule alikuwa ni mke wa mgombea kwa hiyo hata kama ingekuwa wewe mheshimiwa Mnyika lazima mke wako angesimama kidete kuhakikisha unashinda,” alisema Simba.
Akizungumzia uwepo wa asasi zilizoingia nchini kwa malengo mengine lakini hivi sasa zimebadilisha mwelekeo na kuomba kibali cha usajili kwa msajili wa mabadiliko ya ndani waziri huyo, alisema hakuna asasi ya kimataifa iliyoomba kubadilisha maudhui yake.
Kiongozi huyo alisema jukumu la serikali ni kuweka mazingira wezeshi si katika kufikia ruzuku za wafadhili wa nje pekee bali pia katika kupata rasilimali za ndani.
Kwa mujibu wa Simba, serikali tayari imeshaweka mazingira mazuri ya kuhakikisha kuwa inaondoa migongano baina ya asasi za ndani na zile za kimataifa ikiwemo kufikia rasilimali kutoka kwa wafadhili wa nje.
SOPHIA SIMBA APATA MSUKOSUKO BUNGENI
MBUNGE wa Ole (CUF), Rajabu Mohamed Mbarouk, amemjia juu Waziri wa Maendeleo ya jamii, Jinsia na watoto, Sophia Simba kwa kile alichodai ni mjumbe wa bodi ya asasi ya Wanawake na Maendeleo (Wama) ambayo imekuwa ikifanya siasa.
Alisema Mama Salma Kikwete, ambaye ni mke wa Rais Jakaya Kikwete na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM anatumia taasisi hiyo kujiandalia nafasi ya kisiasa kwenye uchaguzi wa mwakani.
Mbunge huyo alitoa hoja hiyo wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ambapo aliwataja wajumbe wengine wa bodi ya Wama kuwa ni Mke wa Rais wa Zanzibar, Mwema Shein, Zakiah Megji ambaye ni Mjumbe wa Nec na Katibu wa Uchumi na Fedha, wote wana CCM.
"Naomba muongozo wako mheshimiwa Spika iwapo Waziri mwenye wajibu mamlaka ya kusimamia mashirika yasiyo ya kiserikali anakuwa mjumbe a bodi ya Wama ambayo ni kinyume na sheria ya NGO ya mwaka 2002... Natoa shilingi hadi Waziri atoe majibu ya kuridhisha," alisisitiza.
Mbarouk alisema Simba ni Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake wa CCM (UWT), naye amehusika katika siasa kwenye Wama huku akiwa mjumbe wa bodi jambo ambalo linaonyesha taasisi hiyo ni mahususi kwa kufanya siasa.
"Tunatambua Wama inapewa misaada mingi kwa jina la Wama na wafadhili wanafanya hivyo wakijua wanasaidia jamii lakini inaonekana ni siasa tu," alisema.
Hata hivyo, katika majibu yake Waziri Simba, alianza kwa kuwashambulia wapinzani kwa kudai kujifanya ni Umoja wa Katiba ya Wananchi kumbe ni wazushi na kwamba ni kawaida kwa wake wa marais kuwa na NGO za kusaidia jamii.
Aidha, Waziri Simba alikiri kuwa Mjumbe wa Bodi kutokana na nafasi yake kama Waziri kuwa malezi wa NGO nchini na kwamba hana maslahi yoyote na taasisi hizo. Hata hivyo, hoja hiyo ilipita kwa kupigiwa kura za ndiyo.
Na Salome Kitomari na Jacqueline Massano, Dodoma

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
1 comment:
Hizi asasi za kijamii za wake wa marais ni za msimu. Huundwa wakati wakiwa Ikulu, muda wao wa kuongoza ukiisha, na taasisi inakufa. Taasisi ya Mama Mkapa iko wapi? Mbona hatuisikii tena? Wafadhili hawatoi pesa kwasababu hawamuhitaji tena Mama Mkapa.
Post a Comment