ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 19, 2014

Warning of strong winds and large waves along the coast

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706 
FAKSI: 255 22 2460735/2460700                                                                 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz                                                            DAR ES SALAAM
Tovuti:  www.meteo.go.tz                               


Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622                                                                       19 Mei, 2014

Taarifa kwa umma: Upepo mkali pamoja na mawimbi makubwa vinatarajiwa   katika maeneo yote ya ukanda wa pwani.

Taarifa Na.
201405-01
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 10 Alasiri
Daraja la Taarifa:
Tahadhari
Kuanzia:
Tarehe
19  Mei, 2014
Mpaka:
Tarehe
21 Mei, 2014
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Hali ya Upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa zaidi ya mita 2.0 inatarajiwa katika ukanda wote wa pwani.
Kiwango cha uhakika:
Wastani (60%)
Maeneo yatakayoathirika
Pwani ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Maelezo:
Hali hii inatokana na kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika nchi kutoka kusini.
Angalizo:
Wakazi wa maeneo yaliyotajwa (hatarishi) wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo pale itakapobidi.

Imetolewa na

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

No comments: