Stori: Musa mateja
BAADA ya kimya kirefu tangu ndoa iliyopagwa kufungwa kati yake na Charles Pai kuyeyuka, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) anayewakilisha vijana Mkoa wa Geita, Vicky Kamata ameibuka na kufunguka mambo mengi lakini kubwa ni kwamba, amefanyiwa sherehe.
BAADA ya kimya kirefu tangu ndoa iliyopagwa kufungwa kati yake na Charles Pai kuyeyuka, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) anayewakilisha vijana Mkoa wa Geita, Vicky Kamata ameibuka na kufunguka mambo mengi lakini kubwa ni kwamba, amefanyiwa sherehe.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, juzi Alhamisi kwa njia ya simu akiwa bungeni Dodoma, Vicky alisema watu wamezungumza mengi kuhusiana na ishu ya ndoa yake kuhairishwa lakini hakuna alisema ukweli.
“Watu wanaongea sana. Wamezungumza mengi lakini mimi ndiye mwenye ukweli. Nawashukuru sana wale ambao wamekuwa upande wangu katika kipindi kigumu nilichopitia.
“Ilifikia hatua baadhi ya wabunge wenzangu wanawake waliamua kunifanyia dinner party (hafla ya mlo wa usiku). Ilinifariji sana, wengine ni watu wazima, mama zangu walinipa moyo sana kwa yaliyotokea.
“Walikuwa wabunge wengi, nakumbuka hata mama zangu, Tibaijuka (Ana – Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi) na mama Kilango (Anne Malecela – Mbunge wa Same Mashariki) walikuwepo,” alisema na kuongeza: “Walinipa moyo, wakaniambia nitulie nifanye kazi. Kila kitu namwachia Mungu. Walinichangia mpaka fedha, kwa kweli nawashukuru sana kwa kampani yao, wote wanajijua, siwezi kuwataja wote.” MADAI YA MUME WA MTU
“Kuna watu wanapakaza kuwa, eti mchumba wangu ni mume wa mtu ndiyo maana tukashindwa kufunga ndoa, siyo kweli. Nakiri kwamba aliwahi kuoa na aliachana na mke wake kisheria tangu mwaka 2012.
“Watu waache kuzungumzia mambo wasiyoyajua. Mimi ndiye ninayeujua ukweli, lakini najua wabaya wangu ndiyo wanaosambaza hayo maneno yasiyo na ukweli,” alisema Vicky. AWACHANA WABAYA WAKE
“Ni vile watu hawaelewi, lakini ukweli ni kwamba kuna baadhi ya wabunge wana uadui na mimi. Hao ndiyo wanaosambaza habari za uongo magazetini. Kuna mwanamke aliibuka, akasema mchumba wangu ni mume wake, haikuwa kweli. “Huyo dada alitumwa na hao wabaya wangu ili wanivurugie mambo yangu ya kisiasa tu. Hizo ni njama za wabunge wasionipenda, ni mchezo mchafu wa kisiasa. Mara nyingi nasema hiyo ni siasa majitaka.
“Kama nilivyokuambia, aliyekuwa mkewe waliachana tena kwa taratibu zote, siye aliyesema kuwa nafunga ndoa na mumewe. Yule dada ni mtu mzuri, ana moyo mzuri, hana makuu sema huyo aliyeharibu shughuli yangu alitengenezwa na wanasiasa wenzangu ili waniharibie na kunivuruga kiakili, nasema wameshindwa.” PAI KUTOROKA NA MICHANGO
“Wamesema mengi, wamenichafua kwa mengi, hadi wamefikia hatua wakasema mchumba wangu ametoroka na michango kiasi cha milioni arobaini – si kweli.
“Mchumba wangu yupo hapa nchini na anaendelea na kazi zake kama kawaida. Lilikuwa zengwe tu lililotengenezwa na baadhi ya wabunge wapinzani wangu ili waniharibie.”
GPL
No comments:
Post a Comment