
Mh. Vicky Kamata aliwasili Bungeni Dodoma na kama ilivyo ada alipokewa vizuri na kila mbunge aliyekutana nae.
Wabunge wengi walimpa pole baada ya
kuugua siku chache kabla ya ndoa yake na kumtakia kila la kheri, huku wengi wakiamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kua Ndoa yake ipo na itakuwepo siku yoyote Mungu akiamua kulitimiza kusudi lake juu ya Mh. Vicky Kamata..
Wakati wabunge wengi wakimuhurumia na kudhani kua kutofungwa kwa ndoa yake kungemgharimu siku nyingi kurudi katika hali ya kawaida,
lakini ilikua ni tofauti kabisa kwa upande wa Mh. Vicky Kamata kwani muda wote alikua na amani na kwamba hakujiskia vibaya kama wengi walivyodhani na ndio maana ilichukua muda mfupi sana na aliweza fika Bungeni na kazi ya kuwatumikia wananchi wake wa Geita na Tanzania kwa ujumla ilianza mara moja na kwamba bado anaamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kwamba Mungu hakosei na anamini Muda si mrefu atafunga ndoa na kila mtu atashuhudia na mkono wa Mungu utasiamama juu ya ndoa yake.
Na anabainisha yote hayo katika wimbo wake mpya "Moyo wa mtu Kichaka" hapo chini. (Picha kwa hisani ya Vicky Kamata blog)
1 comment:
Kila kiumbe kilicho umbwa na Mungu kina haki hapa duniani
ila wanadamu tamaa zinatuponza nakutuaribia utukufu na bahati zote alizotujalia mwenyezi Mungu.
Post a Comment