ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 17, 2014

Kuhusu Wambura Kuenguliwa tena Simba na Kamati ya Uchaguzi


Kamati ya Uchaguzi ya Simba imemuondoa kabisa Michael Wambura katika mchakato wa uchaguzi wa Simba kwa madai kuwa amevunja taratibu za uchaguzi.
Wambura tenaAkiongea na waandishi wa habari leo mchana katika ukumbi wa Serengeti, JB Belmonte Hotel jijini Dar, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Simba Dr. Damas Ndumbaro amesema
Wambura amerudia kosa kwa kufanya kampeni kabla ya wakati kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi.
Kamati hiyo imeeleza kuwa TFF haina mamlaka kikatiba kusimamisha uchaguzi wa Simba kwa hiyo uchaguzi huo utaendelea kama ulivyopangwa kufanyika June 29 mwaka huu.

No comments: