Watanzania
leo wanaelekeza macho na masikio yao mjini Dodoma, kusikiliza Hotuba ya Bajeti
ya Serikali, inayotarajiwa kusomwa saa 10 kamili bungeni na Waziri wa Fedha,
Saada Mkuya Salum.Tayari
Waziri Saada alishaeleza kuwa makadirio ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa
fedha wa 2014/15, unaoanza Julai mwaka huu, yatakuwa Sh trilioni 19.6 kutoka
makadirio ya Sh trilioni 18.2 ya Bajeti inayoisha muda wake.Vipaumbele
vya Bajeti hiyo, kwa maana ya miradi itakayozingatiwa zaidi, ni iliyo katika
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaohusisha sekta sita za Kilimo, Elimu,
Maji, Utafutaji rasilimali fedha, Nishati, Uchukuzi na Uboreshaji wa Mazingira
ya kufanyia biashara na Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano.
Akisoma
mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2014/2015, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, alisema mapendekezo ya mpango huo,
yana vipaumbele vitano.
Cha
kwanza ni miundombinu, kikifuatiwa na
Katika
hotuba hiyo, Watanzania wengi watakuwa makini kusikiliza bidhaa na huduma
zitakazoongezwa kodi, jambo linalotarajiwa kuongeza bei ya bidhaa za huduma
husika katika soko.
Katika
bajeti inayoishia, Serikali iliongeza
kodi kwenye magari makuukuu, bia, vinywaji vikali na baridi ambavyo kodi
imekuwa ikiongezwa kila mwaka na kuwaathiri watumiaji.
Kutokana
na hali hiyo wanywaji pombe na sigara baada ya bajeti ya mwaka juzi ya
2012/2013, walilazimika kutumia fedha nyingi ili kupata huduma hizo kwa kiwango
kile kile katika mwaka huu wa bajeti unaoisha.
Bidhaa
zisizokuwa za mafuta ambazo zilifanyiwa marekebisho na kuongezwa kodi ni
mvinyo, pombe, vinywaji vikali, na sigara.
Ushuru
pia uliongezwa kwenye magari yasiyokuwa ya uzalishaji na yenye umri wa miaka 10
kutoka asilimia 20 mpaka asilimia 25.
Lengo
la Serikali katika hilo, lilikuwa kupunguza uagizaji wa magari chakavu ili
kulinda mazingira na kupunguza ajali za mara kwa mara.
Katika
bajeti hiyo, vijana wa bodaboda walicheka baada ya Serikali kusamehe ushuru wa
barabara kwa pikipiki hizo za biashara.
Moja
ya kivutio kikubwa cha Bajeti inayowasilishwa leo, ni matarajio ya wafanyakazi
kuhusu utekelezaji wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoitoa katika sherehe za
Mei Mosi mwaka huu, ya kuongeza mshahara wa kima cha chini na kupunguza kodi ya
mshahara (PAYE).
Rais
Kikwete alisema Serikali itaendelea kuongeza mshahara wa kima cha chini na
kubainisha kuwa mwaka 2005 alipoingia madarakani, alikuta mshahara wa kima cha
chini ni Sh 65,000 na kukipandisha taratibu hadi kufikia Sh 240,000 cha sasa.
Kuhusu
kupunguza PAYE, Rais Kikwete alisema kusudi la Serikali ni kupunguza kodi hiyo
ya mshahara kutoka asilimia 13 inayotozwa sasa, ifikie katika kiwango cha
tarakimu moja.
Kuhusu
misamaha ya kodi ambayo mwaka huu imekuwa gumzo bungeni, huku wabunge wengi
wakitaka ipunguzwe, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, alinukuliwa akisema
wafanyabiashara na vigogo wanaokwepa kodi kwa kujificha kwenye mwavuli wa
misahama, hawako salama.
“Tutafuatilia kikamilifu kwa kuwa wapo watu
wanaingiza bidhaa wanapewa msamaha, lakini ukija kwenye huduma za jamii unakuta
bidhaa hizo zinauzwa kibiashara,” alisema.
Mwigulu pia alizungumzia ukwepaji kodi na
matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kufafanua kuwa, yatadhibitiwa.
“Bahati nzuri niliyonayo, sikuzaliwa na chembe
ya woga, kwa hiyo kwenye hili hakuna mkubwa wala mdogo, hakuna mtu atagusa
fedha ya umma kwa kukwepa au kwa kutumia vibaya kodi ambayo ilishakusanywa
halafu akapona asiguswe,” alisema.
Mwigulu alisema katika Bajeti ya Serikali ya
2014/2015, yapo mambo ya msingi matano, ambayo yatasimamiwa kikamilifu ili
kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa tofauti na zilizopita.
Mbali na kuondoa misamaha ya kodi, pia makusanyo ya ndani yatatiliwa mkazo
zaidi ili kujenga uwezo wa kujitegemea wenyewe badala ya kutegemea wahisani.
Jambo la tatu alisema ni kuhakikisha Serikali
inapeleka fedha kwenye mahitaji muhimu na kwa wakati, ili fedha za maendeleo
zitumike kama ilivyokusudiwa.
Jambo la nne litakalozingatiwa kwa mujibu wa
Mwigulu, ni usimamizi wa fedha zinazopatikana kwani pamoja na makusanyo kidogo,
lakini pia kuna uvujaji.
“Tunataka fedha inayopatikana na kupangiwa kazi
fulani itumike kwa shughuli iliyokusudiwa. Tutahakikisha tunasimamia na
kudhibiti matumizi yake,” alisema.
Naibu Waziri huyo wa Fedha alisema eneo la tano
ambalo litaangaliwa ni fedha ambazo hazitokani na kodi, bali zinachangwa na
wananchi na wadau wengine katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Alisema eneo hilo ni muhimu mbalo Serikali inaona kuna haja ya kulisimamia vizuri,
ili kuhakikisha fedha za wananchi
zinatumika vizuri.
Kwa upande wa Kenya, hotuba ya Bajeti ya
Serikali ya Kenya, itasomwa na Waziri wa Fedha, Henry Rotich. Katika taarifa
yake kwa wabunge wa Kenya mwezi Machi mwaka huu, Rotich alieleza kuwa Bajeti ya
Kenya kwa mwaka wa Fedha wa 2014/15, itakuwa Shilingi za Kenya Trilioni
1.8.
Nchini Uganda, Waziri wa Fedha wa Uganda, Maria
Kiwanuka ndiye atakayesoma hotuba ya Bajeti ya Serikali ya Uganda kwa mwaka wa
fedha 2014/15.
Kiwanuka ataeleza hatua mbalimbali za kuinua
uchumi, kupunguza kodi mbalimbali na kudhibiti mfumko wa bei.
Hivi karibuni, Kiwanuka alikaririwa akisema kuwa
uchumi wa Uganda unaendelea kukua kwa kasi, lakini siyo katika viwango vya
miaka 1990 na 2000, ambapo ulikua kwa asilimia 7.
Kwa upande wa Rwanda, hotuba ya Bajeti ya
Serikali itasomwa na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda, Claver
Gatete.
Bajeti yote ya Rwanda kwa mwaka 2014/15
inatarajia kuwa Faranga za Rwanda bilioni 1,753. Kwa mujibu wa Shirika la Fedha
Duniani (IMF), uchumi wa Rwanda unatarajia kukua kwa asilimia 6 katika
mwaka wa fedha 2014/15, ukilinganisha na asilimia 4.6 mwaka 2013.
Burundi, Waziri wa Fedha, Mipango ya Uchumi na
Maendeleo wa Burundi, Tabu Abdallah Manirakiza, ndiye atasoma bajeti ya
Serikali ya Burundi kwa mwaka wa fedha 2014/15.
No comments:
Post a Comment