Bryan Daudi akiwa amewasili kwenye ukumbi wa Hampton Inn uliopo College Park kwenye sherehe yake ya kupata komunio ya kwanza iliyohudhuriwa na na ndugu, jamaa na marafiki akiwemo Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula.
Bryan katika picha ya pamoja na mdogo wake Noreen Daudi.
Baba yake Bryan, Baraka Daudi akiongea machache kuwashukuru watu wote kwa kufika kwenye sherehe ya komunio ya kwanza ya mwanae na baadae Bryan aliongea kwa kuanza kuwashukuru wote kwa kufika pia kumshukuru Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula na baadae kuelezea malengo yake ya kufika mbali kwa kufuata mafundisho ya dini aliyopata ikiwemo na lengo la baadae kutumikia kanisani bila kuwa sahau kuwashukuru wazazi wake kwa malezi bora yenye misungi na mwongozo wa dini na kuwakaribisha tena watu wote miaka miwili ijayo atakapopata kipaimara.
Bryan akikata keki.
Bryan akimlisha keki bibi yake.
Kutoka kushoto ni Baba mzazi wa Bryan, Bibi, mdogo wake Bryan, Mama mkubwa wa Bryan Mrs Mary Kalindaga aliyekuja mahususi toka Geneva, Switzerland, Bryan, Baba wa Ubatizo Vitalis Gunda na Mama mzazi wa Bryan katika picha ya pamoja,
Kuoka kushoto ni Flora, Hidaya, Aika na mama mkubwa Mrs Mary Kalindaga.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha na Padri Evod Shao.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi.
2 comments:
bryan is such a cute boy and classic hongereni wazazi wake kwa kumuweka mtoto wenu uptodate
Bryan DAUUUUDIIIIII
Post a Comment