WAKAZI wa kijiji cha Okeseni Chini, Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro, wanalala mapema wakihofia kushambuliwa na kundi la wanyama
aina ya Chui lililovamia kijiji hicho.
Akizungumza kwa njia ya simu jana, mmoja wa wakazi
hao, Pamfill Shayo, alisema hivi sasa wanakijiji hao wanaingia ndani saa
12 jioni na kulala wakiogopa kushambuliwa na chui hao ambao tayari
wameshaua mifugo ipatayo 25.
Alisema kundi hilo la Chui limekuwa likirandaranda katika vichaka
vilivyoko karibu na kijiji hicho na kila giza linapoingia wanajitokeza,
hali inayotishia usalama wa maisha yao.
“Hawa Chui hadi sasa wameua mbuzi, mbwa, paka na kuku. Hali inatisha
uanajua mnyama huyu alivyo na vurugu wakati mwingine wanavamia kundi la
mifugo na kuiua,”alisema Shayo.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Melkadeke Mushi, alikiri kijiji hicho kuvamiwa na wanyama hao.
Hata hivyo, alisema taarifa zimefikishwa kwenye Idara ya Wanyamapori,
hivi sasa wanasubiriwa ili kuwarudisha katika maeneo ya hifadhi ya
taifa.
Na Shehe Semtawa
No comments:
Post a Comment