Baadhi ya akinamama Manispaa ya Morogoro wakikimbiza gari ndogo
lililowabeba watuhumiwa wa kesi ya kula njama na kumtesa Nasra Rashidi
(4) wakati wa uhai wake baada ya kesi yao kughailishwa hadi juni 12
wakati wakipelekwa kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya kuhojiwa upya
kutokana na Nasra kufariki dunia juni mosi mwaka huu.
Kutoka kushoto ni baba mzazi wa mtoto Nasra Rashid, Rashid Mvungi, mama
mkubwa wa Nasra Rashid, Mariamu Saidi na mume wa Mariamu Saidi, Omari
Mtonga wakiwa chini ya ulinzi wakati wakisuburi kusomewa mashtaka ya
kula njama na kumtesa Nasra Rashidi (4) wakati wa uhai wake mkoani
Morogoro.
Mkazi
wa mtaa wa Boma Road, Khadija Amri (55) akiongea kwa jazba mara baada
ya kuwaona watuhumiwa wa kesi ya kula njama na kumtesa Nasra Rashidi (4)
wakati wa uhai wake katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro.
Waandishi
wa habari wakimchukua picha kwa mama mkubwa Nasra, Mariamu Saidi (38)
mara baada ya kufikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro wakati
wa kusikiliza kesi inayomkabili ya kula njama na kumtesa Nasra Rashidi
(4) wakati wa uhai wake.
Askari akifanya kazi ya kuwazuia wananchi waliotaka kumpiga mama mkubwa
wa mtoto Nasra, Mariamu Saidi (38) na kuhamishiwa shemeu nyingine wakati
alipofikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Morogoro kusikiliza kesi
ya kula njama na kumtesa Nasra Rashidi (4) wakati wa uhai wake mkoani
Morogoro.
Mama mkubwa wa Nasra, Mariamu Saidi (38) akifikishwa mahakama ya hakimu
mkazi kusikiliza tuhumu zinazomkabiri katika kesi ya kula njama na
kumtesa Nasra Rashidi (4) wakati wa uhai wake mkoani Morogoro.
Mmoja
wa watuhumiwa wa kesi ya kula njama na kumtesa Nasra Rashidi (4) wakati
wa uhai wake, Omari Mtonga (30) akifikishwa katika mahakama ya hakimu
mkazi mkoa wa Morogoro
No comments:
Post a Comment