RPC wa Iringa, Ramadhani Mungi |
GARI aina ya Scania lenye namba T527 BPQ
na tela namba T 976 BME limechomwa moto kwa makusudi baada ya kushusha na kuuza
mzigo wa mitumba uliokuwemo ndani yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP
Ramadhani Mungi alisema watu sita wanachikiliwa na jeshi hilo wakihusishwa na
tukio hilo.
Mungi amesema askari polisi wakiwa doria
katika maeneo ya Mafinga, wilayani Mufindi Mkoani Iringa walikuta gari likiwa
linaungua bila ya kuwepo kwa dereva wala tingo wake.
Baada ya uchunguzi walimbaini dereva wa
gari hilo kuwa ni Elia Christiani mwenye umri wa miaka 26 na tingo wake Deusi
Gembe Mwenye umri wa miaka 20 kuhusika na tukio hilo.
Alisema watuhumiwa hao waliwasha moto
gari hilo baada ya kushusha kwa magendo
mzigo huo wa mitumba kwa mtu aliefahamika kwa jina la Agrey Mpinga na kukimbia.
Uchunguzi uliofanywa na Polisi unaonesha
suala wizi huo una mtandao mkubwa unaowahusisha watu wengine watu, Masko Buhewa
(53) ambaye ni mfanyabiashara katika kijiji cha Nyololo wilayani humo, Isack
Buhewa (25) na Petro Kipera (26).
Katika katika lingine, jeshi hilo linawashikila
watu wawili wakituhumiwa kujifanya wao ni askari Polisi.
Watu hao ni Bashili Nyakungu (20)
aliyekutwa akiwa amevaa sare za jeshi la Polisi huku akiwatapeli watu kwamba
anatoa nafasi kwa vijana wanaotaka kujiunga na jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment