ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 24, 2014

Doto Mallongo mwanachama hai wa Jumuiya ya waTanzania DMV

Na Ebou Shatry

Mkaazi mkongwe katika Jiji la Washington D.C. Bwana Doto Mallongo siku ya Jumatatu June 23 amefanikisha  kulipa ada yake ya uwanachama hai baada ya kukutana na Jabiri Jongo, ambae ni Mjumbe wa tume ya uchaguzi wa Jumuiya ya waTanzania DMV ili kujianda kwa ajili ya maandalizi ya kinyang'ang'anyiro cha uchaguzi ujao utakaofanyika Julai 21, 2014

Mkazi wa  mkongwe wa DMV bwana Doto Mallongo akimkabizi pesa taslim Bwna Jabiri Jongo ambae ni Mjumbe wa tume ya uchaguzi wa Jumuiya ya waTanzania DMV na kuwa Mwanachama hai wa jumuiya.

Katika harakati hizo za maandalizi ya  uchaguzi uliopangwa kufanyika Julai 20,  mwaka huu, kwa mujibu wa sheria ya katiba ya Jumuiya ya waTanzania DMV, waTanzania wote wanapaswa kuwa wanachama hai ili wajipatie fursa ya upigaji kura na kumchagua kiongozi wanaemtaka 

Bwana Doto kwa uthipitisho wa kufuata sheria hizo za katiba na kuwa mwanachama hai, alisisitiza sana watu kulipa ada ya uwanachama hai ili wapate fursa ya uchaguzi wakupiga kura na kumchagua kiongozi wanaemtaka, Doto Mallongo aliyasema hayo akiwa mmoja wa wanachama wajumuiya jijini hapa anaetaka mabadiliko dhidi ya uongozi uliopita, kwa utekelezeaji wa sheria za katiba ya Jumuiya ya waTanzania DMV

Baada ya kulipa ada yake ya kuwa mwanachama hai, aliwataka tume ya uchaguzi wa Jumuiya ya waTanzania DMV kuwa makini sana na maamuzi binafsi ambayo yanafanywa kwa ukiukwaji wa katiba bila ya kushurutisha pande nyingine, ambapo kwa hivi sasa tayari maswali mengi yameanza kujitokeza dhidi ya ukiukwaji wa sharia katika mchakato wa uchaguzi utakaufanyika mwishoni mwa mwenzi ujao.



10 comments:

Anonymous said...

Yaani DOTTO tangu kipindi choote hicho ulikuwa hujalipa ada, pamoja na ubabe woote unaoleta mjini!! kama si uchaguzi usingelipa hata sent!! hukuwa na sababu ya kutuletea kwenye mtandao wa kijamii ni waTanzania wangapi wako hapa DMV watakaojileta staili yako kujaza blog ya LUK!!!

Anonymous said...

hawana hata office?Sie huku NC tunayo tumewashinda nyie wa DC kutwa maneno tu.

Anonymous said...

DMV AIBU ISIO KIFANI.MALIPO YA UWANACHAMA YANAFANYIKA PARKING LOT.NO RECEIPT ? NYIE WATZ HUKO MNAHITAJI MABADILIKO.

Anonymous said...

Dotto ameonyesha mfano wa kuigwa.Dotto ukigombea,count kura yangu.

Anonymous said...

Hapa DMV ofisi ya jumuiya iko kwenye park na inafanya kazi siku ya nyama choma Tu. Na endapo Una swali au concerns yoyote basi itabidi usubiri hadi wakati huo. Mambo ya kupanga jengo kwa ajili ya ofisi huo muda wala plan haipo kwani budget ipo Tu kwa ajili ya nyama choma na tena kwa wale wasio wanachama na wanachama. Jumuiya DMV- Oyeeeeeee..Dj Luke usiibanie pls

Anonymous said...

Hongera kwa maandalizi ya uchaguzi wa Jumuiya DMV nawatakia mafanikio mema.Abui Junior from sweden

Anonymous said...

Doto acha Ubwanyenye!!

Anonymous said...

doto ni meneja kampeni wa libe inaonyesha hata katiba ya jumuiya haijui. ili uweze kupiga unatakiwa kuwa mwanachama kwa siku 30 kabla ya uchaguzi. yeye amelipia ada june 23,2014 wakati uchaguzi ni july 20,2014. kwa msingi wa katiba ya jumuiya doto hawezi kupiga kura july 20,2014. huyo ndiyo kampeni meneja wa libe. kweli team libe hata katiba hamjui. ttetetetete ahahahhhahaha.

Anonymous said...

doto ni meneja kampeni wa libe inaonyesha hata katiba ya jumuiya haijui. ili uweze kupiga unatakiwa kuwa mwanachama kwa siku 30 kabla ya uchaguzi. yeye amelipia ada june 23,2014 wakati uchaguzi ni july 20,2014. kwa msingi wa katiba ya jumuiya doto hawezi kupiga kura july 20,2014. huyo ndiyo kampeni meneja wa libe. kweli team libe hata katiba hamjui. ttetetetete ahahahhhahaha.

Anonymous said...

wana dmv tunaomba jabir ajiuzulu katika tume ya uchaguzi. sababu anachangia kuvunja katiba kwa kuchukua michango ya watu ili wampigie libe kura. mbaya zaidi anathubutu kuchukua michango nje ya siku 30 kama katiba inavyosema. mfano mzuri ni hapo anachukua mchango wa doto. wana dmv tunaomba tume ya uchaguzi imuamuru jabir jongo kujiuzulu la tutasign petition ya yeye kuondolewa.