Na Ebou Shatry
Mkaazi mkongwe katika Jiji la Washington D.C. Bwana Doto Mallongo siku ya Jumatatu June 23 amefanikisha kulipa ada yake ya uwanachama hai baada ya kukutana na Jabiri Jongo, ambae ni Mjumbe wa tume ya uchaguzi wa Jumuiya ya waTanzania DMV ili kujianda kwa ajili ya maandalizi ya kinyang'ang'anyiro cha uchaguzi ujao utakaofanyika Julai 21, 2014

Mkazi wa mkongwe wa DMV bwana Doto Mallongo akimkabizi pesa taslim Bwna Jabiri Jongo ambae ni Mjumbe wa tume ya uchaguzi wa Jumuiya ya waTanzania DMV na kuwa Mwanachama hai wa jumuiya.
Bwana
Doto kwa uthipitisho wa kufuata sheria hizo za katiba na kuwa mwanachama hai,
alisisitiza sana watu kulipa ada ya uwanachama hai ili wapate fursa ya uchaguzi
wakupiga kura na kumchagua kiongozi wanaemtaka, Doto Mallongo aliyasema hayo
akiwa mmoja wa wanachama wajumuiya jijini hapa anaetaka mabadiliko dhidi ya
uongozi uliopita, kwa utekelezeaji wa sheria za katiba ya Jumuiya ya waTanzania
DMV
Baada
ya kulipa ada yake ya kuwa mwanachama hai, aliwataka tume ya uchaguzi wa
Jumuiya ya waTanzania DMV kuwa makini sana na maamuzi binafsi ambayo yanafanywa
kwa ukiukwaji wa katiba bila ya kushurutisha pande nyingine, ambapo kwa hivi
sasa tayari maswali mengi yameanza kujitokeza dhidi ya ukiukwaji wa sharia
katika mchakato wa uchaguzi utakaufanyika mwishoni mwa mwenzi ujao.

10 comments:
Yaani DOTTO tangu kipindi choote hicho ulikuwa hujalipa ada, pamoja na ubabe woote unaoleta mjini!! kama si uchaguzi usingelipa hata sent!! hukuwa na sababu ya kutuletea kwenye mtandao wa kijamii ni waTanzania wangapi wako hapa DMV watakaojileta staili yako kujaza blog ya LUK!!!
hawana hata office?Sie huku NC tunayo tumewashinda nyie wa DC kutwa maneno tu.
DMV AIBU ISIO KIFANI.MALIPO YA UWANACHAMA YANAFANYIKA PARKING LOT.NO RECEIPT ? NYIE WATZ HUKO MNAHITAJI MABADILIKO.
Dotto ameonyesha mfano wa kuigwa.Dotto ukigombea,count kura yangu.
Hapa DMV ofisi ya jumuiya iko kwenye park na inafanya kazi siku ya nyama choma Tu. Na endapo Una swali au concerns yoyote basi itabidi usubiri hadi wakati huo. Mambo ya kupanga jengo kwa ajili ya ofisi huo muda wala plan haipo kwani budget ipo Tu kwa ajili ya nyama choma na tena kwa wale wasio wanachama na wanachama. Jumuiya DMV- Oyeeeeeee..Dj Luke usiibanie pls
Hongera kwa maandalizi ya uchaguzi wa Jumuiya DMV nawatakia mafanikio mema.Abui Junior from sweden
Doto acha Ubwanyenye!!
doto ni meneja kampeni wa libe inaonyesha hata katiba ya jumuiya haijui. ili uweze kupiga unatakiwa kuwa mwanachama kwa siku 30 kabla ya uchaguzi. yeye amelipia ada june 23,2014 wakati uchaguzi ni july 20,2014. kwa msingi wa katiba ya jumuiya doto hawezi kupiga kura july 20,2014. huyo ndiyo kampeni meneja wa libe. kweli team libe hata katiba hamjui. ttetetetete ahahahhhahaha.

wana dmv tunaomba jabir ajiuzulu katika tume ya uchaguzi. sababu anachangia kuvunja katiba kwa kuchukua michango ya watu ili wampigie libe kura. mbaya zaidi anathubutu kuchukua michango nje ya siku 30 kama katiba inavyosema. mfano mzuri ni hapo anachukua mchango wa doto. wana dmv tunaomba tume ya uchaguzi imuamuru jabir jongo kujiuzulu la tutasign petition ya yeye kuondolewa.
Post a Comment