MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amemtaka mbunge mwenzake, Leticia Nyerere, aache ubunge na akajiunge na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuliko kuendelea kukipigia debe chama hicho akiwa upinzani.
Kauli hiyo ameitoa jana alipokuwa akichangia bajeti ya serikali kwa mwaka 2014/2015 ambapo alisema matendo anayofanya Leticia ya kujipendekeza kwa CCM yatamgharimu kama ilivyotokea kwa wenzake.
Juzi wakati akichangia bajeti hiyo, Leticia alisema serikali ikifanya vizuri, lazima ipongezwe kwakuwa imepeleka maendeleo katika jimbo analotoka.
“Serikali yangu imefanya mambo mengi, imeniletea maji, walimu katika jimbo langu la Kwimba, ni lazima tuipongeze si kila wakati tunailaumu humu ndani,” alisema.
Katika mchango wake jana, Mdee, alisema jukumu kubwa la upinzani ni kuikosoa serikali na kuonyesha mbadala katika masuala mbalimbali na si kuisifia kwa kutekeleza wajibu wake wa kuwahudumia wananchi.
“Serikali inapata fedha kutokana na kodi za wananchi, inalazimika kupeleka maji, barabara na huduma mbalimbali kwa lazima si hiyari, tunapoikosoa tunatimiza wajibu wetu kama yenyewe inavyotekeleza inapowahudumia wananchi.
“Leticia Nyerere anaweza kwenda CCM, kwakuwa Rais Kikwete ana nafasi mbili za uteuzi wa wabunge, lakini lazima ajue waliojipendekeza CCM wamepigika sana hivi sasa, aachie ubunge aende huko kwakuwa ana mapenzi nao,” alisema.
Mdee alisema kuwa Leticia anaiaibisha kambi ya upinzani inayofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha serikali inaboresha huduma inazozitoa kwa wananchi.
“Upinzani si lelemama, kama anafikiria CCM ni kuzuri zaidi ni vema akaenda huko kuliko kubakia hapa pasipomfaa,” alisema.
CREDIT:UDAKUSPESIALLY
3 comments:
N amimi namtaka alivue kufu hilo akasaidie jimboni kwake ambapo kuna watu wasiojiweza hata kwa mlo mmoja.Mwenzie Leticia havai gold ya thamani ya Dollar alfu sabini.
Wacha upuuzi wewe mchangiaji namba 1 yaani na akili zako timamu roho inakutoka kwa mkufu tu wakati wanaowasababishia watu/wananchi matatizo makubwa kila kukicha wapo na wanazidi kuwepo kwa kupeana vyeo na kuanzisha miradi mbalimbali, Umebaki kutolea macho vitu personal na kujisahau kabisa kama nawe unahusika kama unajiweza kwa kutoa msaada... Huyu Mama Leticia hana lolote maana kitendo cha kuishabikia CCM ni kuishiwa tena kwa kupitiliza, Haileti maana kama jimbo lake lina maji,umeme halafu jimbo linalopakana nae halina hata kisima/bwawa la uhakika kunyweshea mifugo na hata elimu ni Majanga haswaaaa
Kama vipi aache ubunge na kuhamia CCM kabla hajarudi huko Marekani kufanya kazi kwa masaa
*Hongera sana Mbunge wangu/kioo Halima Mdee
Wewe ni nani ambae unajitoa akili..???? Huyu mbunge analipwa kama wengine na pia haufahamu ni lini kanunua huo mkufu na hata hivyo hivi ni urembo tu kwa wanawake wote hivyo kama Leticia hataki kuvaa dhahabu ni maamuzi yake na huyu Halima ni mapenzi yake pia au wewe umekuwa mtunga sheria kwa kuingilia mambo Personal ya watu.? Tafakari sana kijana(Usilaumu ulipoangukia ila laumu pale ulipojikwaa)
Post a Comment