ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 3, 2014

HAPPINESS MAGESE: NATESEKA KUTOKUPATA MTOTO

Happiness Magese (35), alikuwa akifanya kazi zake za uanamitindo nchini Afrika Kusini chini ya Kampuni ya Ice Model Management na alikaa huko kwa miaka nane kabla hajahamia katika Jiji la New York, nchini Marekani ambapo amesaini mkataba na Kampuni ya Ford Models mpaka sasa hivi. Ana miaka minne na tayari ameshaongezewa miaka miwili zaidi ya fani hiyo ya uanamitindo duniani.
Happiness Millen Magese akijifuta machozi wakati akielezea alivyoteseka kupata mtoto. 
Ijumaa iliyopita, Happiness alifika katika ofisi za Global Publishers zilizopo Bamaga, Mwenge, jijini Dar es Salaam na moja kwa moja alizungumza na waandishi wa habari kupitia safu hii ya Live Chumba cha Habari ambapo aliongelea mengi kuhusiana na maisha yake na fani nzima ya uanamitindo.
Baadhi ya maswali na majibu kati ya Happiness na waandishi wa Global Publishers yalikuwa kama ifuatavyo;

Mwandishi: Tuambie Millen Magese Foundation ni nini, kazi zake ni nini na lengo lake ni nini?
Happiness: Ni foundation ambayo inashughulika zaidi na mambo ya elimu, afya na kumuinua mwanamke.
Happiness Magese akistorisha juu ya mafanikio aliyoyapata kupitia sanaa ya urembo.

Katika mambo ya elimu nimejikita zaidi kumuweka mwanafunzi au yule mtoto ambaye yupo shuleni awe katika mazingira mazuri ya kujisomea.

Siyo hapa tu Tanzania nimeanzisha nchi nyingi sana kwa sababu katika education kwangu its very personal, naiangalia kwa ukaribu sana kwani ilinikumba mimi mwenyewe wakati nikiwa mdogo na katika maisha yangu yaliyopita ndiyo maana naamua kuwa karibu na hawa viongozi wa baadaye, sijaanza leo tangu nikiwa Miss Tanzania niliweza kutembea mikoa zaidi ya 20 Tanzania.
Happiness Magese katika moja ya shughuli zake za monyesho ya mavazi nchini Afrika Kusini.


Mtwara na Lindi nimeguswa sana ndiyo mana niliahidi siku nikirudi Tanzania nitaweza kujenga shule au kuendelea kutoa misaada zadi.

Baada ya miaka 12 nilivyorudi bado nilikuta hali ni ileile, watoto bado walikuwa wakikaa chini nikapelekwa shule nyingine ambayo ni kajumba kadogo kalikuwa ka udongo. Jambo hili ningependa nilifuatilie zaidi na kuanza kusaidia nimeanza na darasa moja na ndani ya darasa moja yapo madarasa matatu, na la nne linaendelea tutawapa updates wiki hii.
Happiness Millen Magese akiwa 'mtoni' katika matanuzi na moja ya mashosti zake.


Mwandishi: Millen Magese Foundation inatoa huduma gani kwa upande wa afya? 
Happiness: Katika suala la afya tumejikita zaidi katika hali ya kiafya ya maumivu ya mwanamke katika hedhi ambayo inajulikana kitaalam kama ‘Endometriosis’.

Ugonjwa huu umeshanikumba na napenda niweke wazi kwa maana ni vyema mtu akianza mapema hawezi kuwa na matatizo yaliyonikumba.

Nimeshafanyiwa upasuaji mara 12 na mirija yangu yote imeziba, upande wangu mmoja wa ovary haufanyi kazi. Ile ndoto yote ya mimi kama mwanamke kupata mtoto kwa njia ya kawaida imetoweka. 
Nisingependa kuona wanawake wengine wanakwenda njia niliyopitia na ndiyo mana nipo hapa Tanzania ili kuweza kuliongelea zaidi na kuiomba hata serikali, vyombo vya habari watu wote kujitolea kuweza kumsaidia mwanamke huyu ambaye anaweza kuwa kama mimi.
Magese akipoza koo wakati akilonga na Global.
Ukimsaidia mwanamke utakuwa umesaidia dunia nzima. Mwanamke ni nguzo katika nyumba yoyote ni suala ambalo linapaswa kuongelewa na wababa, wakaka na viongozi kila sehemu.
Nimepanga kutoa semina mbalimbali kwa wanawake, ikiwezekana kufungua hospitali maalum ya wanawake itakayotibu ugonjwa huu.

Mwandishi: Tangu umeanza kuutibu ugonjwa huu wa Endometriosis, umetumia kiasi gani?
Happiness: Nilianzia Afrika Kusini ambako nilifanya operesheni 10, mbili nimefanyiwa Marekani. Gharama ya Afrika Kusini ilikuwa ni randi 35,000 (sh milioni 5,500,000) kwa Marekani ilikuwa ni dola 6,000 (sh. milioni 9,958,000).

Halafu kuna vitu ambavyo unatakiwa uvitumie kwani kuna kuwekewa mayai na unachomwa sindano 63 kwenye tumbo, kila siku unachomwa sindano tatu kwa siku 22 na kila siku unaamshwa kwa ajili ya kufanyiwa Ultrasound, nadhani unaona maumivu ni kiasi gani unayapata. Kwa bahati mbaya mwili wangu uliweza kuzalisha mayai matatu kwa sababu ovary yangu moja haifanyi kazi wakati wengine wanazalisha kuanzia saba mpaka 15.
Magese akiwa mbele ya jarida la kimataifa la Complete Fashion.

Endometriosis kwangu imekuwa sugu ndiyo maana msishangae siku nikienda Italy, Marekani au sehemu yoyote kuasili mtoto, hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ndivyo alivyonipangia.

Mwandishi: Changamoto zipi unakumbana nazo katika fani ya uanamitindo?
Happiness: Changamoto yangu kubwa ilikuwa ni afya yangu.

Nilikuwa sijui lini nitakuwa okey, lini nitafanyiwa upasuaji na lini nitarudi kwenye kazi yangu maana ukiondoka leo zinakuja sura mpya zaidi ya 1000 unashindwa kujua kama utarudi na kuwa top. Nashukuru nilipata viongozi wazuri wa kunisimamia na kuniongoza mpaka nimejulikana kama Happiness Magese na kuwa mwanamitindo maarufu.

Nawaomba waajiri wote muwaangalie watu wa namna hii na mkishamfahamu ana ugonjwa wa Endometriosis mpeni ushirikiano sana.
Mwandishi: Kwa nini suala la fani nzima ya urembo linaonekana kama uhuni?

Happiness: Katika fani nzima ya urembo ni kwamba unavyoonekana tayari unakuwa ni ghali. U need to be taken care, u need to be good, to be presentable ambayo unaitangaza linakofanyika Shindano la Miss World. Watu wanadhani kuwa mrembo lazima uwe mhuni kwa sababu mrembo ni lazima awe msafi muda wote, awe anatumia gharama.

Wengi hujiuliza sasa pesa anazipata wapi mpaka anakuwa mrembo namna hiyo, ina maana waandaaji ndiyo wanampa pesa? Mimi nilipokuwa Miss Tanzania nilipata sapoti kubwa kutoka kwa wazazi wangu.
Credit:GPL

3 comments:

Anonymous said...

GARI YOYOTE IKIPATA TATIZO HUPELEKWA CAR DEALER, NAE AKISHINDWA HUULIZWA MANUFACTURE.MWENYE KULIUNDA HATASHI-
NDWA KABISA. PIA MANUAL YA GARI ISIPOZINGATIWA GARI HUFA KABISA. SASA DADA MAGESSE,HAPPYNES UNAJIJUA WEWE KULIKO WENGINE WANAVYOKUJUA. KAMA HUKO UJANANI HASA KWENYE TEEAGE ULITOA SANA MIMBA KWA MADAWA BASI HIYO SABABU KUBWA TENA MTOTO WAKO HAWEZI KURITHI. ALL IN ALL WEWE UMEUMBWA NA MUNGU, HIVYO MWOMBE YEYE AKUSAIDIE SABABU YEYE NI MANUFACTURE [CREATOR] WAKO.

Anonymous said...

Millen dear you can get pregnant with Endo. I have had it for 10 years and had surgery twice for it. I have a beautiful 21 month old son and my husband and I are trying for another baby now. I had to take Clomid during 5 days of my cycle but it only took one round and I got pregnant with my son. I started Clomid again and now I am anxiously waiting until I can take a pregnancy test. Good Luck dear.

Anonymous said...

HIIII Unalia, kwani hujijui yaliyofanyika huko nyuma ukiutaka uzuri sasa unacholia nini, Kugawa uligawa, hujampata mtu wa kukupa ujauzito wapo endelea kuwatafuta utapata tu usililie wa wenzio, dddhhhh, Nenda kamuone daktari na upate ushauri. Hapo kila binadamu anasikitika sio wewe pekee.