Video ya Erick Bahunde alipokuwa akiingia kwenye holi ilikofanyika harambee yake na alianguka mara tu alipoanza kutembea kuelekea kwenye holi pia kwenye video hii aliongea na kutoa shukurani zake kwa wote waliofika na ambao hawakufika kwani nia ilikuwepo nisimalize kila kitu we Bofya Play ya Video umsikilize mwenyewe na kama utakuwa umeguswa na mateso ya Erick ambayo hakuyatarajia na yanaweza kumkuta mtu yeyote popote pale tuma pesa Checking Account # 3900681515 Routing # 054001220 Wells Fargo Bank Jina: Elisha Bahunde. Erick anatanguliza shukurani.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi.
Uchungu wa mwana ajuae mzazi, huyu ndiye Mama mzazi wa Erick aliyekuja toka Tanzania kuja kumuuguza mwanae,
Meza kuu ikiongozwa na Erick Bahunde, mpendwa wetu aliyepata ajali na kukatika miguu na mkono siku ya Jumapili June 8, 2014 Silver Spring, Maryland kwenye harambee ya kumchangia iliyoongozwa na Katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn, Amos Cherehani kwa ushirikino na Faraja Isingo
WanaDMV wakiendelea kutoa michango yao
Faranga ikiendelea kuchangishwa,
Wadau mbalimbali wanaDMV wakifuatilia harambee.
Mwongozaji wa harambee Said Mwamende akiwakabidhi waratibu wa harambee hiyo katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Amos Chereheni (kati) na Bwn. Faraja Isingo (kushoto)
Waratibu wa harambee wakimkabidhi Erick Bahunde harambee ya WanaDMV.
Mchungaji Malekela akiongea jambo kabla ya harambee kuanza.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV akiongea machache na kusisitiza mshikamano wa wana DMV hasa kunapotokea mmoja wetu anapopata matatizo kama Erick usisite kujitokeza na kulaani vikali wale wote waliotoa maoni ya kukatisha tamaa wenzao na kuwavunja nguvu wakati hawajui taratibu za malipo anazolipwa mtu kama Erick na mpaka taratibu zikamilike huchukua muda, na kusisitiza daima tuwe wepesi kusaidia badala ya kujifanya mafundi wa kupiga domo na kuandika comment. Katibu wa Jumuiya ya Watanzania DMV Amos Charehani aliongea mapema wakati wa ufunguzi wa harambe nae kukemea jambo hilo.
WanaDMV wakifuatilia harambee.
Juu na chni ni wanaDMV wakiwasili huku wakibadilishana mawili matatu kabla hawajaingia kwenye ukumbi wa harambee.
Juu na chini wanaDMV wakiwa ndani ya ukumbi wakifuatilia harambee
Rais wa Jumuiya ya Watanzania Idd Sandaly akitangulia kumpapole Erick Bahunde mkono wa pole na baadae kutoa mchango wake
Katibu wa Jumuiya Amos Cherehani ambaye pia ni maratibu wa harambee ya Erick akitoa mkono wa pole na kuchanga chake,
Musa Linga akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Alex Kassui akimpa mkono wa pole Erick na baadae kutoa mchango wake.
MwanaDMV akitoa mkono wa pole na baadae kuchanga mchango wake.
Mzee Safari (kushoto) na Danny Star wakitoa pole kwa Erick na baadae kutoa mchango wao.
Jacob Kinyemi akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Dada Rehema akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Joseph akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Dada Muna akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Dada Harriet akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Dada Joha akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
mama yetu MwanaDMV akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Baraka Daudi akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Julius Manase akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Richard Mawenya akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Dada Farida akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
JB akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Dada yetu MwanaDMV akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Dada yetu mwanaDMV akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Kijana wetu mtoto wa mwanDMV akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Dada yetu Salma akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Dada yetu Salma na vijana wetu wtoto wa wanaDMV wakipata picha ya kumbukumbu.
Tano Ladies wakiwakilisha
Liberatus Mwang'ombe na mtoto wa mwanaDMV katika picha ya pamoja na Erick nabaadae wakatoa mchango wao.
Mchungaji Samson na mwenzie ambao ndio wanaotoa usafiri kwa Erick popote anapoenda wakipata picha ya pamoja.
Quize akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Makeo akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Abuu Shatry akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake.
Kessy akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Fela akitoa mkono wa pole na baaadae kuchanga mchango wake
Fela na Kessy Janabi wakipata picha ya kumbukumbu.
Minada ikiendelea
Mzee Safari ambaye yupo kwenye kamati ya Uchaguzi akisisitiza wanaDMV wajiunge na Jumuiya wachague viongozi wao ambao ni haki yako ya msingi kufanya hivyo.
Asha Nyang'anyi akisisitiza wanaDMV kujiunga na chama na pia kuitangaza sherehe ya Tano ladies itakayofanyika weekend hii. fuatilia matangazo yao kwenye Vijimambo na mitandao mengine.
15 comments:
mnamoyo wa huruma sana wa kuwasaidia watu wana dmv lakini pia wajanja nyinyi yani basi tuu
DJ LUKE OMBI LANGU MAALUM NAOMBA UTOE HILI TANGAZO MARA KWA MARA ILI WATU WAENDELEE KUCHANGIA HICHO KIASI NI KIDOGO SANA NA NI AIBU KUBWA KWETU SISI WANA DMV...KUMBUKA HUYU MTU AMEKUFA NUSU MWILI NA ANACHANGIWA KIASI HIKI KIDOGO NAMNA HII NA MAREHEMU NDIYO NYINGI KABISA KWA KWELI INATIA AIBU NA TUNAOMBA YALE MAJINA YA WALIO CHANGA YAWEKWE KWENYE BLOG KABISA ILI TUJUANE WA KUSAIDIANA PALE INAPOTOKEA TATIZO. NA WATU WANAPASWA KUKUMBUKA HIVI ERICK ALIPOSOMA COMMENTS KAMA ZILE ZA KUKATISHA TAMAA ANAPATA PICHA GANI???JAMANI TUMUOGOPE MUNGUUUUU
DJ LUKE PLS OVER PLS USIIBANIE HII
jamani pole sana,kweli mwanadamu angekuwa anajua linalokuja mbele yake,kwani nimemsikiliza huku kaka nikabaki nakujiuliza mwenyewe,siku zote yeye overtime hafanyi hiyo siku ameamua kwenda kufanya ndio anakutana na tatizo. kweli Mungu anamakusudi yake nani wakushukuliwa kwa kila jambo
Hivi Nyie wana DMV mbona sio ni tamko sijuwi tano lady sijuwi kanisa lolote limetoa mchango???hovyooo kweli bwana siwaoni wale matajiri aw DMV version one sijuwi ushuzi mtupu mbona sijaona ubishoo wa bure hovyooo DMV nimewazarau sanaaaa .wewe luka usibanie maana Wewe ....Tamko mbona hamjachangisha wakati mnajuwa dini ya kislam ni kusaidiana Au Nyie nikufuturisha tuuu na nyama choma na majungu??? nitarudi badae
ANONYMOUS # 2. UMETOA WAZO ZURI LA KUTAKA MAJINA YATOLEWE ILA HUHITAJI YATOLEWE KWANI MAADAMU WATU WALIOFIKA NA KUSHIRIKI KTK HILO TUKIO NATUMAINI MNAWAFAHAMU KWA MAJINA KAMA SI KWA SURA. HIVYO HAO NDIYO MNAPASWA KUSHIRIKIANA NAO KWA SHIDA NA RAHA. HAKUNA EXCUSE YA KUTOFIKA KWENYE TUKIO HILI MUHIMU LABDA UWE ULIKUWA UNAUMWA HOI NA UMELAZWA AU UMESAFIRI MASAFA MAREFU. NA HILI LIWE FUNDISHO KWENU NA SISI WOTE TUNAODHANI KILA ANAYEKUCHEKEA NA KUALIKANA KWENYE MAPARTY( HARUSI , , BABY SHOWER ETC) NI RAFIKI YAKO WAKATI WA SHIDA AU WA RAHA.?
ANONY,# 2 NAKUBALIANA NA WEWE KUWA NI VIZURI KUWEKA MAJINA YA WALIOCHANGA ILA MAJINA SI MUHIMU ILA MUHIMU ZAIDI NI WATU WALIOFIKA HAPO NA KWANI SI RAHISI KUJUA KILA MMOJA KWA MAJINA NA HAKUNA EXCUSE YA KUTOFIKA LABDA UWE ULIKUWA UNAUMWA HOI AU UMESAFIRI SAFARI YA MBALI . KITU AMBACHO NIMEKIONA HAPO DMV MNA UMOJA WA MANENO NA SI MATENDO. WATU MNAALIKANA KWENYE MAPARTY HARUSI, BABY SHOWER, NYAMA CHOMA NA KADHALIKA NA MNAJAA KUPITA KIASI ILA MWENZENU KAOMBA MSAADA MNAKAA MBALI. HILI LIWE FUNDISHO KWENU NINYI WANA DMV NA WENGINEO KWA UJUMLA KUWA WAKATI WA SHIDA UTAMJUA NANI RAFIKI KAMILI NA RAFIKI MNAFIKI NA SI KILA ANAYE KUITA RAFIKI AU NDUGU NI MTU ATAKAYEKUSAIDIA UKIWA NA SHIDA NA SIKU ZOTE SHIDA HAINA MWENYEWE.
MDAU
CANADA
Naungana na mdau hapo juu ni kweli kabisa kwani taasisi binafsi, jumuiya, makanisa na misikiti hawakutuma mwakilishi ktk kumchangia huyu kijana au ni kusimama kwenye majukwaa kuhubiri umoja, amani na upendo wakati hata hamkujitokeza kwenye tukio muhimu kama hili.
Na hapo DMV si ndiyo Washington DC kwenye ubalozi wetu mbona sijaona hata mwakilishi? au walifanya kazi weekend...??
Yaani kweli mmetia aibu hadi watu wataogopa sasa kujichanganya, kwani la kutokea likitokea ujue ni la kwako na usitegemee watu.
Ubalozi wa Tanzania hapa Marekani ulialikwa rasmi na wali-confirm kuwa watafika lakini hakuna hata Diplomatic Officer wa ubalozi aliyekuja kwenye harambee hii. Hii inamanisha kuwa ubalozi na wanajumuiya ni vitu viwili tofauti kabisa na ubalozi uko hapa DC kwa maslahi ya serikali siyo ya wanajumuiya. Matukio kama haya yalitakiwa kuratibiwa na Ubalozi na siyo kwa kujitolea kama uongozi wa Jumuiya ambao haupokei posho yoyote kamwa wafanyakazi wa ubalozi wanaolipwa mamilioni.
Nilichojifunza mimi kutokana na tukio hili ni kuwa, kutokana na mahudhurio hafifu ya watu 43 kati ya watu Zaidi ya 400 walio hapa DMV watanzania hatuko pamoja, watanzania tumegawanyika na hatujaliani hata kidogo. Ubalozi wa Tanzania hapa Washington DC hauna faida yoyote na watanzania badala ya kutuonesha picha za sherehe mbalimbali za kutanua kwa kutumia pesa za serikali pale ubalozini. Kuna haja ya kutia mgomo ili blogs zote hapa DMV zisionyeshe matukio yanayoendelea kwenye ubalozi wetu ili wabadilike.
Jumuiya ya Watanzania DMV ni ya watanzania ambao mambo yao hayajanyoka, watanzania maskini ambao hawana makaratasi, kazi zao ni hizi hizi za mabox, matahira, kuosha magari, kukata nyasi, baby seating, delivery, dreva taxi cabs na zingine ambazo siyo rasmi. Mambo yako yanaponyoka kama yalivyowanyokea watu wa World Bank, Ubalozi wa Tanzani, Voic e of America , DC na Federal Government then Jumuiya inakuwa useless. Ndiyo maana huwezi kuwaona watanzania walio na kazi nzuri kwenye shughuli za kimaskini kama hii! Nani toka Voice of America alikuja kwenye harambee ya kimaskini kama hii? Nani alikuja toka Ubalozini kwenye mambo ya michango kama haya?
Msidanganyike wana Jumuiya acheni kutegemea harambee, nendeni shule, oeni au oleweni ili mpate karatasi na mambo yatawanyokea ili muache kutegemea mambo ya harambee. Wana DVM msilaumu mtu, jilaumuni ninyi na uvivu wenu. Pesa iliyochangwa inatosha maana imetoka kwenye mifuko ya maskini ambao wanapata $8.00 per hour.
Anonymous June 9, 2014 at 11:00 PM umeandika upuuzi mtupu afu hueleweki kajifunze kuandika kwanza tunapata tabu kuelewa point yako ni nini hasa.
Swala ni wewe umechanga? sio unaanza kusema mbona fulani hajachanga, wewe umechanga?
Mdau wewe ndio mtu wa majungu kwa kuanza kuandama jumuiya za DMV...mambo kama haya hayana dini na hakuna haja ya tamko au makanisa kujitangaza jinsi yanavyosaidia watu...wana tamko na mapadre wamekuwa mbele kumsaidia na kumtembelea kaka yetu tokea apate ajali. Sasa kabla kujaanza kushutumu watu jiulize wewe mwenyewe umemsaidia nini huyu kaka yetu. kama huamini hivi muulize ni kina nani wanampa kampani kila siku kama sio vijana wa tamko....mijitu mingine sijui imefata nini nchi za watu...haibadiliki kama kaniki
Wee mchangiaji wa mwisho usituchafuie hali ya hewa, Waliohudhuria na kuchangia kiasi cha pesa ni waislamu wa Tamco rudi kaangalie picha.. Rais wetu Iddy ambaye ni mtu wa TAMCO peke yake kachangia mamia kununua vitu kwenye mnada, TANO LADIES walichangia doti za kanga za OBAMA, kahawa na tende na zikapigwa bei ya juu kuchangia mfuko weye unayeandika ndo wale mliokuwa mnamkebehi kaka wa watu aliyenusurika maisha nakupoteza viungo vyake muhimu vya mwili..
"LEO KWAKE KESHO HUWEZIJUA ITAKUWA KWAKO"
Wewe navyosema tamko Au kanisa naimanisha jumuiya ya tamko Au kanisa mbona mliweza kuchangia mafuriko ya Zanzibar Kama tamko why sijaona vilemba vya tamko ?? Iiddy kuepo ni Sawa yeye ni raisi wa jumuiya lazima awepo japo hakutoa hiyo idea .Sasa unauliza Kama nimechanga ??Ndiyo nimechanga ndiyo maana nimeuliza wako wapi hizo taasis zenu kwenye shida .Nielewe vizuri sana nataka Erick achangiwe sio mnamchangia mtu amekufa tuu Au maharusi na nyama choma mnatakiwa kumchangia Huyu kaka anahitaji mchango wacheni kubisha wakati ukweli mnaujuwa . Watanzania hampendi kuambiwa ukweli duuuh
DJ LUKE pLS RUSHA TENA HATUJAMALIZA MDAHALO WETU.
Hapa DMV tumechanga kwa mambo mengi... Misiba, harusi, pati, maafa bongo na mengi bila kujali dini. Ukae ujue hapa DMV kuna jumuiya za dini, kikabila, kitaaluma, kisiasa na majungu kama ya mdau mchafua hewa.
Sasa kama unataka kila jumuiya iwakilishwe katika kila kitu hili jambo haliwezekani kwa wale wanaokuja kwenye mikusanyiko hawavai lebo za utambulisho Bali huja kama binaadamu. Acha kuwa angalia watu kwa dini, kabila, au vyeo vyao katika jamii kwani yatakushinda na utajenga uadui usiokunufsisha.
Post a Comment