ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 10, 2014

HONGERA JWTZ KWA KUFANIKISHA OPERESHENI YA WAASI WA M23.



Vikosi vya Tanzania vilivyokuwa vikilinda amani nchini DRC Congo kwa kuondoa kikundi cha M23 vimeanza kurejea nchini.

Jumla ya askari wetu mashujaa 850 waliondoka tarehe 07 June 2013 kwa kuagwa na Mhe Rais Jakaya Kikwete katika hafla iliyofanyika Msangani,Kibaha.

Katika operesheni hiyo ya
ushirikiano wa pamoja na askari toka Namibia,Malawi na Afrika Kusini.FIS ikiongozwa na Jenerali Mtanzania James Mwakibolwa ilifanikiwa kusambaratisha kundi la M23 ambalo bila kificho chochote lilikuwa na nguvu kubwa ya baadhi ya nchi2 jirani.

Mara tu baada ya kufika kwa askari watiifu wa Tanzania katika ardhi ya Congo,wacongo wengi walianza kupata matumaini waliyoyakosa kwa muda mrefu.Na hatimaye kundi lile la waasi la M 23 na mengineyo kama la FDLR kwa sasa yamesambaratika na kufanya hali ya amani nchini Congo kuwa safi,kitendo ambacho kwa upande mmoja kimetusaidia sana watanzania ambao tumekuwa kimbilio la wakimbizi ambao ndani yake wamekuwa wakifanya uhalifu sehemu kadhaa kama Kigoma,Geita nk.

Hawa hawa wakimbizi ndio waliosababisha serikali kuunda Operesheni iliyoacha majonzi kwa watanzania wengi ilhali matukio yale yalifanyw ana wageni (Wakimbizi).

JWTZ inaondoka Congo kukiwa na hali nzuri ya amani,wamama na watoto wa Congo wanalia kwa kuondoka Jeshi letu shupavu!Jeshi ambalo halijawahi kushindwa hata siku moja katika operesheni yoyote mfano Operesheni Kumekucha dhidi ya Wareno mwaka 1960, Operesheni TEGAMA huko Msumbiji dhidi ya Majeshi ya Rhodesia na Afriak Kusini (mwaka 1975-1980),Operesheni Safisha Msumbiji dhidi ya RENAMO mwaka 1986-1988,Operesheni dhidi ya mamluki waliovamia kisiwa cha Seychelles mwaka 1981-1982,Operesheni demokrasia Comkoro Machi 2008,Operesheni hii ilitumia masaa yasiyozidi 14 kumalizika! na kwa hakika ulikuwa ushindi wa hali ya juu licha ya wavamizi wale kutoa vitisho kwa majeshi yetu.Operesheni ile ilimwondoa adui Kanali Bakar aliyejitangazia ufalme ndani ay visiwa vya Anjouan.

Zipo pia Operesheni za kulinda amani chini ya UN mfano za Liberia,Lebanon na Darfur,kote huko JWTZ imefanya operesheni kamambe na imefanikiwa kutimiza majukumu yake.

JWTZ pia ndio iliyoutimua utawala wa Nduli Idd Amin aliyejaribu kufanya uvamizi ndani ya ardhi ya watanzania na kuchakazwa vibaya katiak vita iliyoitwa Vita ya Kagera mwaka 1978,Amin licha ya kusaidiwa na marafiki zake nchi ya Libya iliyokuwa na vifaa vya kisasa zaidi vya kivita,aliteketezwa vibaya sana na JWTZ iliyokuwa chini ya Amiri Jeshi Mkuu Mwalimu Julius K. Nyerere.Kwa hakika JWTZ ni jeshi imara na lenye uwezo mkubwa wa kulinda mipaka ya Tanzania na kulinda dhidi ya maadui zake.Kwa hakika wanastahili pongezi kubwa JWTZ.na ni ufahari mkubwa kuwa na jeshi lenye weredi,utiifu na uwezo kama la JWTZ.

Karibuni tena mashujaa wetu katika ardhi ya nyumbani.

2 comments:

Anonymous said...

Bwana Muandishi,
hawa jamaa hawaendi nyumbani. Hawa jamaa JWTZ wanabadilishana kwa kimombo inaitwa " rotation"...yaani wanarudi baadhi na wengine wanapelekwa...hivyo Idadi ya JWTZ under FIB katika kikosi cha MONUSCO iko pale pale...hadi kitapoeleweka kabisa...Kwa lugha nyingine bado JWTZ itaendelea kuwa DRC until further notice, from UN Security Council,..


Mdau

Anonymous said...

Ndugu Mwandishi: Hilo Shavu la Weledi wa JWTZ, nidhamu ya Wanajeshi wetu, kujituma na uzalendo - ni sifa za haki, zinazolifanya JESHI LETU kuwa moja ya Majeshi yanayoheshimika sana, siyo Afrika pekee, bali Duniani. Tatizo langu na taarifa yako ni kuwa, kwa sababu ya kutojitahidi kidogo tu kupata taarifa sahihi, umepotosha kabisa na kuufinyanga ukweli! Iko tofauti ya wazi baina ya "relief" au "rotation" na "repatriation, withdrawal" au neno lolote jingine lakini linalotumika kueleza hali ya kuondoka Jeshi husika bilakurejea katika eneo lavita! Umeikosea sana narrative yako! Ukitaka uhakika, kama uko Dar, mbona hummtafuti Msemaji wa Jeshi akiupe picha? Na kama uko Marekani au kwingineko Magharibi.... Pale UN tunao Ubalozi Kamili wa Kudumu wa Tanzania na Mwambata Jeshi wetu anayehusika moja kwa moja na suala hilo! Nakushauri uongeze bidii ya kutafuta taarifa sahihi kabla hujaandika! Hapo umeupotosha umma wa Wasomaji.