ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 10, 2014

ILIVYOKUWA KESI YA WALIOMNYANYASA MTOTO WA BOKSI, NASRA MVUNGI HUKO MOROGORO



Mtonga Omar (30) ( kulia) ,mkazi  wa Mtaa wa Azimio, Kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro na mkewe Mariam Said (38) ( kati kati) pamoja na Baba Mzazi wa Mtoto Nasra ,  Rashid Mvungi (47), mkazi wa Lukobe  na mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wakisubiri hatma ya kesi yao  ndani kizimba katika  chumba cha wazi cha Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa huo; wanakabiliwa na  mashitaka mawili  la  kula njama na ukatili kwa mtoto Nasra Rashid (4), kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 12, mwaka huu.


Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Morogoro waliofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro,  kwa ajili ya kusikiliza kesi inayowakabili watuhumiwa watatu wa mtoto wa boksi , Mtonga Omar (30)  na mkewe Mariam Said (38) ambao ni wakazi wa Mtaa wa Azimio, Kata ya Kiwanja cha Ndege ,pamoja na Baba Mzazi wa Mtoto Nasra ,  Rashid Mvungi (47), mkazi wa Lukobe na mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro  , leo , wakiwazomea wakiwa ndani ya gari dogo walipokuwa wakiondoka Mahakamani hapo ,wakikabiliwa na  mashitaka mawili ya awali ya   kula njama na ukatili kwa mtoto Nasra Rashid (4), kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 12, mwaka huu.  ( Picha zote na John Nditi).

No comments: