Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya wakimsikiliza RPC
MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI “PRESS CONFERENCE” TAREHE 19.06.2014.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU WAWILI
WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 04:30 ALFAJIRI WALIONEKANA NA
WALINZI WA USIKU WA ENEO LA SOKO KUU LA TUNDUMA LILILOPO KATIKA KATA NA TARAFA
YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA WAKIWA NA SILAHA BUNDUKI NA KUWATILIA MASHAKA KUWA
WANA NIA YA KUFANYA UHALIFU YAANI UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.
WALINZI AMBAO
WALIKUWEPO KATIKA ENEO HILO WALITOA TAARIFA KWA ASKARI POLISI WALIOKUWA DORIA
AMBAO WALIFIKA MARA MOJA KATIKA ENEO HILO. KUTOKANA NA TAARIFA HIZO MSAKO MKALI
ULIANZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA HAO.
MNAMO MAJIRA
YA SAA 05:00 ALFAJIRI YA LEO ASKARI
POLISI WALIKUTANA NA WATU WAWILI WALIOWATILIA SHAKA KUTOKANA NA JINSI
WALIVYOVAA KULINGANA NA MAELEKEZO YALIYOPEWA NA WALINZI. MMOJA KATI YA
MAJAMBAZI HAYO ALIKUWA AMEVAA JAKETI KUBWA JEUSI NA MWINGINE AKIWA AMEBEBA
MFUKO MKUBWA, WAKATI WAKIJARIBU KUWASIMAMISHA WATU HAO WALIANZA KUKIMBIA NA
MMOJA KATI YAO ALIYEKUWA AMEVAA JAKETI ALIPOFIKA UMBALI WA MITA 20 ALITOA SILAHA BUNDUKI NA KUANZA KUFYATUA RISASI OVYO
AKIELEKEA UELEKEO WA ASKARI.
BAADA YA KUONA
HIVYO, ASKARI WALIJIBU NA KATIKA MAJIBIZANO HAYO YA KURUSHIANA RISASI KATI YA MAJAMBAZI NA ASKARI POLISI,
JAMBAZI MWENYE SILAHA ALIPIGWA RISASI UBAVUNI NA KUFARIKI DUNIA, HIVYO KUFANIKIWA KUKAMATA BUNDUKI MOJA AINA YA AK-
47 YENYE NAMBA 592058 IKIWA NA RISASI
25 KWENYE MAGAZINE.
MTUHUMIWA
MMOJA ALIFANIKIWA KUKIMBIA NA MARA BAADA YA KUUPEKUA MWILI WA MAREHEMU
KILIKUTWA KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA CHENYE JINA JOSEPH THADEI KAPINGA, MKAZI WA MAFIGA, MOROGORO ALIYEZALIWA MKOA
WA RUVUMA – SONGEA VIJIJINI TAREHE 07.09.1971.
KATIKA TUKIO
HILO, HAKUNA MADHARA KWA WANANCHI/ASKARI YALIYORIPOTIWA KUTOKEA, UPELELEZI
UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA MTUHUMIWA ALIYEKIMBIA PAMOJA NA MTANDAO
WAO WA UJAMBAZI.
KATIKA
TUKIO LA PILI:
MWANAMKE MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SUZANE MHENDWA (45) MKAZI WA UHAMILA WILAYANI MBARALI AMEUAWA KWA KUCHOMWA KISU
KIFUANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LAZARO
KATENDE.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01:00 KATIKA KITONGOJI CHA CCM,
KIJIJI CHA UHAMILA, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO NI MZOZO ULIOTOKEA KATI YA MAREHEMU NA
MTUHUMIWA WAKIWA NYUMBANI AMBAPO KIINI CHAKE KINACHUNGUZWA.
MAREHEMU NA MTUHUMIWA NI NDUGU WANAOISHI NYUMBA MOJA.
MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII/WANAFAMILIA KUTUMIA NJIA ZA BUSARA KATIKA KUTATUA
MIGOGORO KATIKA FAMILIA HASA KWA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUKA
MATATIZO. AIDHA ANATOA WITO KWA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO
MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA TATU:
WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA
1. THERESIA HINGI (65) NA 2. MARY KIZITO (26) WOTE
WAKAZI WA IGURUSI WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA BASI LA KAMPUNI YA
USAFIRISHAJI – NEW FORCE LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 952 CGU AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA YAHAYA ABDALAH (39) MKAZI WA DSM.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 18.06.2014 MAJIRA YA SAA
18:00 JIONI KATIKA KIJIJI CHA IGURUSI, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO,
BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA
BASI HILO LILILOKUWA LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI LILIGONGA GARI T. 954
AMH AINA YA FUSO LILILOKUWA
LIKIENDESHWA NA DEREVA TUPA ANYOSISYE
(32) MKAZI WA KIWIRA –TUKUYU, KISHA
KUACHA NJIA NA KUWAGONGA WATEMBEA.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE WANNE
WALIJERUHIWA KATI YAO ABIRIA MWANAUME MMOJA NA WANAWAKE WATATU WATEMBEA KWA
MIGUU WOTE WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. PIA MIILI YA MAREHEMU
IMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA
BASI, AMBAYE AMEKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA
KUZINGATIA ALAMA NA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI
ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO
MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imetolewa
na:
[AHMED Z.
MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
|
No comments:
Post a Comment