Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe kwa tiketi ya Chama cha Wananchi
(CUF) Ismail Jussa Ladhu amehoji uhalali wa mbio za Mwenge wa uhuru
zinazofanyika kila mwaka nchini kote na kusema asili yake ni Tanzania
Bara.
Jussa alisema hayo wakati akichangia wizara ya
uwezeshaji wananchi, ustawi wa jamii maendeleo ya wanawake vijana na watoto ambayo pia hujishughulisha na mbio za Mwenge kitaifa.
Akifafanua zaidi alisema mbio za Mwenge wa Uhuru asili yake Tanzania Bara na zilianzishwa na chama cha TANU kilichokuwa kikipigania uhuru kwa wananchi wa Tanganyika.
Alisema chama cha Afro shirazi Pary ambacho kilikuwa kikipigania uhuru kwa upande wa Zanzibar hakikutumia mbio za Mwenge wa uhuru katika harakati zake, kiasi ya kuhoji kwa nini mbio hizo zinaihusisha Zanzibar.

'Mheshimiwa mwenyekiti nataka ufafanuzi kuhusu mbio za Mwenge wa Uhuru zinatija gani kwa upande wa Zanzibar....najuwa mbio za uhuru zililetwa na chama cha TANU kilichokuwa kikipigania uhuru kwa wananchi wa Tanganyika na hapa Zanzibar Afro Shirazi haikuwa na mbio hizo'
alisema Jussa.
Alishangazwa na kusema siku hizi kumekuja utamaduni kwamba miradi mingi ya maendeleo lazima ifunguliwe katika kipindi cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Jussa alitaka ufafanuzi huo wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Uwezeshaji ambayo ndiyo inayoshughulikia masuala ya mbio za Mwenge wa uhuru baada ya kuondolewa katika masuala ya vyama vya siasa.
Mapema Jussa alisikitishwa na Wizara ya uwezeshaji ambayo imejikita zaidi kutoa mikopo kwa vijana kwa muelekeo wa uhusiano wa vyama vya siasa kinyume na malengo ya wizara hiyo.
Alisema baadhi ya majimbo ya uchaguzi ambayo yamechukuliwa na wapinzani yamekuwa yakikosa mikopo ya uwezeshaji kwa vijana, kitendo ambacho hakikubaliki katika mikakati ya kuwaendeleza vijana na kuweza kujiajiri.

'Mheshimiwa mwenyekiti nataka Waziri ajekuniambiya mikopo ya kuwawezesha vijana kujiajiri utaratibu wake na utoaji wa mikopo ukoje...yapo malalamiko kwamba baadhi ya majimbo ya uchaguzi mikopo hiyo haipatikani'
alisema Jussa.
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi akiwemo Salmin Awadh Salmin
wa jimbo la Magomeni alitaka apewa mchanganuo wa upatikanaji wa mikopo
ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika jimbo lake huku akisema
haridhishwi.
Lukwangule
No comments:
Post a Comment