Rais Jakaya
Kikwete leo anatarjia kufanya kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma
kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti Kuu, bungeni kesho.
Kikao hicho
cha Baraza la
Mawaziri kinakaa huku kukiwa na vuta ni kuvute katika
Kamati ya Bajeti ya Bunge ya kupitisha vifungu mbalimbali vinavyoonekana
kuleta utata kwenye bajeti hiyo imeendelea kuisumbua kamati hiyo
ambayo inaongozwa na Mwenyekiti, Andrew Chenge.
Wakati Wabunge wakihoji sababu ya serikali kuendelea kutegemea
wafadhili katika bajeti yake badala ya kukusanya mapato ya ndani,
wamehoji pia matumizi yasiyoyalazima kuendelea kuwekwa kwenye bajeti
hiyo.
No comments:
Post a Comment