Duniani vituko haviishi!
Huko Florida, jamaa mmoja aliyejibandika cheo anachokijua yeye cha Kipolisi na kuanza kufanya kazi kama polisi, alijikuta akimsimamisha Sheriff wa kweli mpelelezi aliyekuwa akiendesha gari lisilo na utambulisho wa kipolisi.
Kijana huyo, Matthew Lee McMahon, 20, alitumia taa maalumu za rangi ya bluu (mara nyingi kwa pamoja na nyekundu), zinazotumika juu ya magari ya polisi wa Marekani kuliashiria gari lolote kusimama kwa ajili ya ukaguzi, kulisimamisha gari la Sheriff mpelelezi, Chance Anderson.
"Nilipaki pembeni ili kukabiliana na mhusika. Wakati huo, yeye alipaki gari lake
pembeni yangu pia. Akanitizama 'kwa kejeli vile' na kuninyooshea kidole," alisema Shefiff Chance akiiambia First Coast News kuhusu mkasa huo uliotokea St. Augustine.
"Nilistaajabu, kwanza, kwa kuona kuwa Afisa wa usalama barabarani anathubutu kunisimamisha," alisema Chance na kuongeza, "Sisi ni kitengo kikubwa, lakini nawafahamu wengi wa maafisa wetu wa usalama."
Kiroja kinapendeza zaidi kwani moja ya kazi na majukumu ya Sheriff Chance ni kukamata watu wanaojifanya kuwa maafisa wa usalama. Ni kama vile kondoo alijipeleka kwenye midomo ya chatu!
Sheriff Chance amekuwa akiifanya kazi hii kwa miaka 10 na kwa muda wote huo anasema, kamwe, hajawahi kukutana na kiroja kama hiki cha mtu ama afisa yeyote aliyekosea na kumsimamisha.
Mtuhumiwa alikamatwa na kuswekwa ndani kwa makosa ya kuhadaa kuwa ni afisa wa polisi na kuwasha taa za bluu pasina ruhusa kisheria. Aliachiliwa kwa dhamana ya $5,500.
Vituko Duniani, haviishi!

No comments:
Post a Comment