Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbrod Slaa
----
DK.
Willbroad Slaa "Sifikirii kuelekeza nguvu zangu kwenye kuwania urais
2015 wapo watu wengi wenyesifa ktk kundi la UKAWA.Kila kitu kitafanywa
kwa wakati muafaka,kazi iliyopo mbele yangu ni kupigania umoja wetu wa UKAWA ili kuleta ushindani wa kweli katika uchaguzi 2015.
Akizungumzia
hatua ya UKAWA kususia Bunge Maalumu la Katiba Dk. Slaa alisema umoja
huo uko sahihi kwani umesimama upande wa wananchi, niaheshimu uamuzi wa
Viongozi wangu Mh Freeman Mbowe Prof Ibrahim Lipumba na James Mbatia.
UKAWA
imebeba maoni ya wananchi na suala la kutengeneza Katiba sio suala la
rais,serikali wala chama chochote bali ni la wananchi.
Serikali
ina viongozi vigeugeu kwa sababu ni wao ndio waliosaini rasimu ya
Katiba mpya, lkn cha ajaabu wao ndio wanageuka na kutaka yajadiliwe
mambo ambayo hayamo ndani ya rasimu ya Tume ya Jaji Joseph
Warioba."
Chanzo:Mtanzania Juni 11-2014
No comments:
Post a Comment