Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Jaji Mstaafu Eusebia Munuo (kushoto) akifunga rasmi Kikao cha Ishirini na Sita cha Bodi ya Taifa ya Parole kilichofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli, Jijini Mwanza(kulia) ni Katibu wa Bodi hiyo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja.
Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Magereza (aliyesimama) ambaye pia ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Bodi ya Taifa ya Parole, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Clement Keenja akitoa hoja ya Maboresho ya Sheria ya Parole Nchini kabla ya kumalizika kwa Kikao cha Ishirini na Sita cha Bodi ya Taifa ya Parole(kushoto) ni Mjumbe wa Sekretarieti, Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Wajumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole(hayupo pichani) wakati wa kufunga rasmi Kikao cha Ishirini na Sita cha Bodi ya Taifa ya Parole kilichomalizika leo Juni 27, 2014 katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli, Jijini Mwanza.
Mjumbe wa Bodi ya Taifa ya Parole Nchini, ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Nchini, Bw. Francis Stolla (Kushoto) akiteta jambo na Katibu wa Bodi ya Taifa ya Parole, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) mara tu baada ya kumalizika kwa Kikao cha Ishirini na Sita cha Bodi ya Taifa ya Parole kilichofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mwanza Hoteli Jijini Mwanza(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).



No comments:
Post a Comment