ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 15, 2014

KIKUNDI CHA WAFUGAJI WA NG'OMBE WA KISASA WAAHIDIWA MKOPO NA BENKI YA COVENANT‏

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya wanawake ya Covenant Bi. Sabetha Mwambenja akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiongea na kikundi cha wafugaji wa ng’ombe wa kisasa cha Kata ya Somangila kiilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, kuhusiana na mradi wa ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa maziwa unaovihusisha vikundi vitatu vya kata hiyo ambapo wafugaji hao watapata mkopo wa kuendeleza mradi huo kutoka Covenant Bank.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya wanawake ya Covenant Bi. Sabetha Mwambenja akitoa mfano wa spoko za beiskali kwa kikundi cha wafugaji zaidi ya 45 (hawapo pichani) wa Kata ya Somangila kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, kuhusiana na mradi wa ufugaji wa ng’ombe wa kisasa wa maziwa. Benki hiyo inategemea kutoa mkopo kwa kikundi hicho ili kiweze kuendeleza ufugaji huo. Kulia ni mtunza Hazina wa Kikundi hicho Jumanne Hussein.
Mratibu wa kikundi cha wafugaji wa Ng’ombe wa kisasa Kata ya Somangila Kigamboni jijini Dar es Salaam, Getruda Mpelembe (kulia) akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Covenant Bi,Sabetha Mwambenja,Baada ya kuongea na kikundi hicho kuhusiana na maswala ya mradi wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa wa kisasa ambapo kikundi hicho kitanufaika na mkopo kutoka benki ya Covenant kwa ajili ya kuendeleza mradi huo wa ufugaji. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Covenant Bi, Sabetha Mwambenja akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiongea na wanakikundi cha ufugaji cha Somangila kilichopo Kigamboni Dar es Salaam, alipotembelea kikundi hicho kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mradi huo wa ufugaji wa ng’ombe wa kisasa wa maziwa ambapo kikundi hicho kitanufaika na mkopo kutoka benki ya Covenant.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Covenant Bi. Sabetha Mwambenja akitoa mfano wa beiskali wakati alipokuwa akiongea na kikundi cha wafugaji Ng’ombe wa kisasa cha Kata ya Somangila Kigamboni jijini Dar es Salaam, kuhusiana na mradi huo.Benki hiyo inategemea kutoa mkopo kwa kikundi hicho ili waweze kuendeleza ufugaji huo. Kulia ni Mratibu wa Wafugaji wa Ng’ombe wa Kata ya hiyo Getruda Mpelembe na katikati ni mtunza Hazina wa Kikundi hicho Jumanne Hussen na Kushoto ni Mwenyekiti Taifa Wajasiriamali Dk. Dauda Salmin.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya wanawake ya Covenant Bi, Sabetha Mwambenja akisisitiza jambo kwa kikundi cha wafugaji wa Ng’ombe wa kisasa wa Kata ya Somangila cha Kigamboni jijini Dar es Salaam, alipofanya ziara na kuongea na kikundi hicho kuhusiana na swala la ufugaji huo. Benki hiyo itatoa mkopo kwa kikundi hicho ili kiweze kununua ng’ombe wa maziwa.

No comments: