Katika kipengele cha Kolabo Bora (Best Collaboration) nominees walikuwa ni 'Number One' (Remix) (Tanzania/ Nigeria), Amani ft Radio na Weasel- 'Kiboko Changu' ( Kenya/ Uganda), Mafikizolo ft May D - 'Happiness' ( Afrika Kusini/ Nigeria), R2bees ft Wizkid - 'Slow Down' (Ghana/Nigeria) na Uhuru ft DJ Buckz, Oskido, Professor, Yuri Da Cunha - 'Y-tjukutja' (Afrika Kusini/Angola) ambapo mshindi alikuwa ni Uhuruft DJ Buckz,Oskido na wengine. Diamond aliambulia patupu katika vipengele vyote viwili alivyoshiriki.
Katika kipengele Mwanamuziki Bora wa Kiume nominees walikuwa ni Anselmo Ralph ( wa Angola), Davido (Nigeria), Donald (Afrika Kusini) , Wizkid (Nigeria) na Diamond Platnumz (Tanzania) ambapo mshindi alikuwa ni Davido kutoka Nigeria.
Diamond alikuwa anawania tuzo mbili lakini hajafanikiwa kushinda kati ya hizo.
Tuzo ya Best Collabo ilitangazwa awali na imechukuliwa na Uhuru ft DJ Bucks,Oskido,Professor,Yuri Da Cunha na wimbo wa Y-tjukutja.
Lakini sio mbaya…
Credit:GPL



No comments:
Post a Comment