Madai mapya ya ufisadi yameibuka
dhidi ya shirikisho la soka duniani FIFA kuhusiana na utata
uliosababisha taifa la Qatar kupewa rukhsa ya kuandaa michuano ya kombe
la dunia ya mwaka 2022.
Gazeti la Sunday Times kutoka Uingereza limesema
kuwa
limepata stakhabadhi zinazoonyesha ambavyo aliyekuwa afisa wa
shirikisho la soka nchini Qatar Mohammed bin Hammam, aliwalipa mamilioni
ya madola maafisa wa soka kwa madhumuni ya kuiunga mkono Qatar kuandaa
michuano hiyo mwaka mmoja kabla ya uamuzi kutolewa.
Bwana Hammam amekataa kujibu madai hayo mapya.
Lakini mwandishi wa michezo wa BBC amesema kuwa
huenda shinikizo zikatolewa dhidi ya FIFA kufanya kura mpya ya kuandaa
michuano hiyo ya mwaka 2022.
Jarida la Sunday Times , lilifichua ambavyo
mamilioni ya dola zilikabidhiwa maafisa wa shirikisho hilo kupitia kwa
akaunti zao pamoja na kuwepo ushahidi wa barua pepe kuhusu mawasiliano
yaliyokuwepo, shughuli hiyo ilipokuwa inafanyika.
Inaarifiwa Mohamed Bin Hammam aliwalipa dola
milioni 5 maafisa wa FIFA ili waweze kuunga mkono Qatar wakati kura ya
nchi itakayoandaa kombe la dunia 2022 ilipofanyika.
Qatar imekanusha madai hayo.
Lakini kulingana na nyaraka zilizopatikana na
Sunday Times na ambazo BBC imeweza kuona, ni bayana kuwa Bin Hammam,
mwenye umri wa miaka 65, alianza kuwarai maafisa wa shirikisho hilo
kupigia kura Qatar mwaka mmoja kabla ya kura yenyewe kufanyika.
Stakabadhi hizo zinaonyesha ambavyo, Bin Hammam
alikuwa anawalipa maafisa wa soka barani Afrika ili kununua ushawishi
wao waweze kuunga mkono Qatar.
Hata hivyo, Qatar imekanusha vikali madai hayo
ikisema kuwa Bin Hammam hakuwahi kuwa na jukumu la kuunga mkono azma ya
Qatar kutaka kuandaa kombe la dunia 2022 na kwamba hakuwa anapigia debe
Qatar kivyovyote
BBC
No comments:
Post a Comment